Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Geita,Elisha Lupuga akitangaza hatua zidi ya watumishi saba ambao wamekutwa na tuhumza za utoro kazini pamoja na wizi. |
Baadhi ya madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Geita wakiwa kwenye kikao cha tatu cha baraza hilo. |
Baraza la Halmashauri ya Wilaya ya Geita imewafukuza kazi watumishi saba
kutokana na kuwa na makosa ya utoro kazini , Udanganyifu na
wizi wa fedha na rasilimali za umma ikiwa ni pamoja na Kushindwa
kuwasilisha mapato ya serikali na Kutokuwajibika.
Mamlaka ya Baraza la
Madiwani imepewa nguvu ya kisheria kuwawajibisha watumishi wa Halmashauri
isipokuwa walimu na wale wanaoteuliwa na Mhe. Rais au Waziri mwenye dhamana kwa
mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na.8 ya mwa ka 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho
na Sheria Na.19 ya mwaka 2002, kifungu cha 6 (6).
Akitoa adhabu hiyo
kwenye ukumbi wa Mikutano Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Elisha Lupuga
amesema Kwa mujibu wa kanuni ya 42(2) na kanuni ya 43(2) ya Kanuni
za Utumishi wa Umma za mwaka 2003, aina ya makosa na adhabu zimeainishwa katika
nyongeza Na.1 na nyongeza Na. 2. kwamba adhabu ambazo zimeainishwa ni pamoja na
kufukuzwa kazi ,kupunguziwa mshahara au
kushushwa cheo.
“Hivyo kamati
imejiridhisha na kuona wanastahili adhabu ya kufukuzwa kazi kutokana na
kukiukwa sheria ya ajira” Alisema Lupuga.
Mwenyekiti Lupuga
amewataka watumishi ambao ni watoro na si waaminifu, waadilifu
na wezi na hawana nidhamu kwenye Utumishi wa Umma wajipange la sivyo
hawatabakia kufanya kazi ndani ya Halmashauri ya hiyo kwani Hawatavumiliwa
kutokana na vitendo hivyo.
Hata hivyo kwa upande
wake Diwani wa Nyawilemelwa,Method Gaspeli amesema maamuzi ambayo yamechukuliwa
na baraza hilo yako sawa kwani yatawasaidia watumishi wenye tabia za namna hiyo
kujirekebisha.
Sanjali na hayo Mkuu
wa Mkoa Huo Mhandisi Robert Gabriel amelitaka baraza hilo kuwa na mkakati wa
kuainisha mradi kwa kila mwaka ambao utasaidia kuingiza mapato kwenye
halmashauri hiyo.
No comments:
Post a Comment