Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana,
Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na waandishi wa habari
juu ya Ufafanuzi wa Hoja za ofisi yake zilizoainishwa katika Ripoti ya Mthibiti
na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Mwaka wa fedha unoishia Juni 30, 2018
Bungeni Dodoma.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano ulioandaliwa na
Idara ya Habari Maelezo, Kwa Mawaziri walipokutana kutoa ufafanuzi kwa baadhi
ya hoja zilizoainishwa katika Ripoti ya Mthibiti na Ukaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali kwa Mwaka wa fedha unoishia Juni 30, 2018
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana,
Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akiteta jambo na Waziri wa Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.William Lukuvi wakati wa mkutano na waandishi
wa habari Dodoma Aprili 23, 2018.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana,
Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na waandishi wa habari
juu ya Ufafanuzi wa Hoja za ofisi yake zilizoainishwa katika Ripoti ya Mthibiti
na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Mwaka wa fedha unoishia Juni 30, 2018
Bungeni Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu
Mhe. Jenista Mhagama amemuagiza Msajili wa vyama vya Siasa kuchukua hatua kwa
vyama vinavyokiuka sheria na miongozo ya vyama vya siasa.
Ametoa kauli hiyo leo (Aprili 23, 2018)
alipokuwa akitoa maelezo ya ufafanuzi juu ya hoja za ofisi yake, zilizoainishwa
katika Ripoti ya Mthibiti na Ukaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Mwaka wa
fedha unoishia Juni 30, 2018 alipokutana na waandishi wa habari Bungeni Dodoma.
Waziri Mhagama ameelekeza kuhakikisha vyama
vyenye mapungufu upande wa hesabu zao basi wawasilishe kwa Msajili wa vyama
ndani ya wiki 3 hadi 4.
“Namtaka Msajili wa Vyama achukue hatua za
Kisheria pasi kusita kwa chama chochote kinachokiuka sheria ya vyama vya siasa
Na. 2 ya mwaka 1992”.alisema Waziri Mhagama
Aidha amemtaka Msajili wa Vyama vya siasa nchini
kuhakikisha anaweka miongozo na mpango kazi ili vyama vilivyozoea kutowasilisha
hesabu zao viache mara moja kwa mujibu wa sheria.
Waziri Mhagama aliongezea kuwa taarifa ya
Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ilibaini mapungufu kadhaa katika
uendeshaji wa vyama vya siasa ikiwemo; Upungufu katika hesabu zilizowasilishwa
chini ya viwango vya Kimataifa vya uandaaji wa hesabu katika sekta za umma na
baadhi ya vyama kushindwa kuwasilisha hesabu zao kwa CAG kwa ukaguzi
Pamoja na hayo alibainisha kuwepo kwa vyama vya
kisiasa visivyotumia rejista ya mali za kudumu ambapo vyama vinne
ikiwemo;CHADEMA, NLD,ADC na Demokrasia Makini havina Daftari la kudumu la mali
zao ikiwa ni kinyume na sheria zilizopo.
“Msajili wa Vyama nakuagiza kutoa maelekezo kwa
kila chama cha siasa chenye usajili wa kudumu kuwa na regista ya mali zake
ndani ya wiki tatu kuanzia leo kwani kukosa daftari la mali za kudumu ni
kinyume na kifungu Na.14(1)(b)(ii) ya sheria ya vyama vya siasa Na.5 ya mwaka
1992.”alisisitiza Waziri.
Sambamba na hilo Waziri alimtaka Msajili wa
Vyama vya siasa kuhakikisha vyama vyote vinafuata miongozo yote ya kihasibu ili
kuondokana na mapungufu ya kukosekana kwa nyaraka za malipo kama
ilivyobainishwa na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ambapo alibaini vyama
vitatu kati ya tisa vina nyaraka pungufu ikiwemo CHADEMA, SAU na ADC.
“Msajili wa vyama ahakikishe vyama vya siasa
vinatekeleza miongozo yote kihasibu pamoja na kanuni za fedha, ambazo
zinaelekeza nyaraka ziwe na viambatisho sahihi kwani ripoti ilibainisha vyama
vitatu vilikuwa na malipo yenye nyaraka pungufu zenye thamani ya shilingi
735,978,559 ambapo ni kinyume na miongozo ya kihasibu na kukosa uhalali wa
malipo hayo.”alisisitiza Waziri Mhagama.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA
WAZIRI MKUU)
No comments:
Post a Comment