Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na
Spika wa Bunge la Afrika ya Mashariki, Mhe. Martin Ngoga kabla ya
mazungumzo yao, Bungeni mjini Dodoma, Aprili 23, 2018. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Spika
wa Bunge la Afrika ya Mashariki,Mhe. Martin Ngoga, Bungeni mjini Dodoma
Aprili 23, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha
ya pamoja na Spika wa Bunge la Afrika ya Mashariki, Mhe. Martin Ngoga (watatu
kushoto) baada ya mazungumzo, Bungeni mjini Dodoma, Aprili 23, 2018. Wengine
pichani ni Wabunge wa Bunge la Afrika ya Mashariki, kutoka kushoto
ni Dkt. Abdullah Hasnuu Makame, Fancy Nkuhi na Mariam Ussi Yahya. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
"Miradi hiyo ambayo kwa sasa inatekelezwa kwa
kasi si kwamba inachochea ukuaji wa uchumi wa Tanzania, bali hata wa nchi
nyingi za jirani kwa kuwa nazo zitanufaika na miradi hiyo kwani si nchi zote
zina bandari".
Dkt. Ngoga ameyasema hayo leo (Jumatatu, Aprili 23,
2018) alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Bungeni
mjini Dodoma.
Amesema tayari wamejadili ripoti iliyotokana na
ziara iliyofanywa na wabunge hao katika upande wa korido ya kuishi na korido ya
kaskazini ambapo wametoa mapendekezo yatakayofanyiwa kazi na baraza la
mawaziri.
"Tayari tumeshajadili miswada miwili inayohusu
Itifaki ya Sarafu Moja ambayo ni mswada wa taasisi ya Fedha na mswada wa
Takwimu yote ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya mwaka 2017."
Pia Spika huyo amesema wamefurahia uwepo wao nchini,
ambapo mbali na shughuli zao za kibunge pia kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma wameshiriki kampeni ya kukijanisha Dodoma kwa kupanda miti
1,000 kwenye eneo la Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
Kwa upande wake, Waziri Mkuu amesema amefarijika na
uamuzi wa Bunge la EALA kufanya vikao vyake katika nchi wanachama kwa sababu
unatoa fursa ya kujua mazingira ya nchi hizo pamoja na maendeleo yake.
Amesema nchi wanachama wanamatumaini makubwa na
bunge hilo katika kuimarisha na kuboresha maendeleo ya mataifa yao, hivyo
amewatakia mjadala mwema.
Katika hata nyingine, Waziri Mkuu amewakaribisha
wabunge hao na marafiki zao kuja kuwekeza kwenye sekta mbalimbali nchini
ikiwemo ya viwanja, utalii, kilimo na madini.
Kwa mara ya kwanza vikao vya Bunge la Afrika
Mashariki, (EALA) vinafanyika Dodoma katika ukumbi wa Bunge wa Msekwa ulipo
ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Vikao hivyo vilianza Aprili
17, 2018 na vinatarajiwa kumalizika Aprili 29, 2018.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
41193 - DODOMA.
JUMATATU, APRILI 23, 2018.
No comments:
Post a Comment