Baadhi ya washiriki
mafunzo hayo kutoka wizara mbalimbali na vyuo vikuu wakifuatilia mafunzo ya
namna ya kutumia mfumo huo.
|
Shirika la Maendeleo
la Umoja wa Mataifa (UNDP) linaisaidia Tanzania kuwa na mfumo bora wa
kukusanya na kuhifadhi taarifa za hewa ya ukaa nchini ili taarifa hizo ziweze
kutumika katika mipango mbalimbali ya kusaidia kukabiliana na mabadiliko ya
tabia nchi pamoja na kuwa na taarifa sahihi za mchango wan chi katika
kukabiliana na tatizo hilo.
|
Akizungumza na
Waandishi wa habari wakati wa mafunzo kwa wadau wakuu wa mpango huo na namna ya
kutumia mfumo huo katika kukusanya taarifa hizo mtaalamu wa miradi inayohusu
nishati na mabadiliko ya tabia nchi kutoka UNDP tawi la Tanzania Bwana Abbas
Kitogo amesema mfumo huo utaiwezesha Tanzania kuwa na takwimu sahihi za hali ya
hewa ya ukaa na namna tunavyopambana katika kuipunguza
Ameongeza kuwa kwa
sasa Tanzania hatuna taarifa sahihi na rasmi sana pale inapotakiwa kueleza
mchango wetu kama taifa katika kutatua changamoto hiyo na hivyo kushindwa kujua
kama nchi tufanye tuongeze nguvu wapi au tufanye nini katika kusaidia jitihada
hizo za dunia
Aidha amebainisha kuwa
kupitia mradi huo wa kujenga uwezo wa serikali katika kujenga mifumo ya jinsi
ya kuzia hewa ukaa Tanzania wameamua kutoa mafunzo kwa wadau mbalimbali kama
vile wizara na vyuo vikuu lengo likuwa ni kuwawezesha wataalamu wa serikali
kuwa na uwezo wa kukusanya taarifa zinazohusiana na mabadiliko ya tabia
nchi na kuzitolea taarifa kule zinakotakiwa.
‘’Tunatakiwa kutoa taarifa kwa
umoja wa mataifa ule mpango maalumu wa hewa ukaa na mbadiliko ya tabia ya nchi
tunazalisha hewa kiasi gani na mipango yetu ya kupunguza ni kiasi gani na namna
ambavyo kama nchi tunaweza kupambana na tatizo hilo hivyo ni muhimu mfumo huu
wa taarifa uwepo maana kwa sasa hatuna’’ Alisema Kitogo.
Amesema kuwa Wataalamu
wametungenezea mfumo GG inventory System ambao utakuwa katika hali
ya taarifa lakini pia kama tovuti maalumu ambayo itakuwa inasimamiwa ofisi ya
makamu raisi lakini watakaokuwa wanaifanyia kazi ni kituo cha kitaifa cha
kufuatilia kaboni kilichopo Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA
maana wao ndio wana utaalamu wa kufanya kazi hii.
Ameongeza kuwa kwa
kuweka mfumo huo SUA utawezesha wanafunzi pia wanaosoma hapo kuweza kujifunza
na kuwa na uwezo kuutumia mfumo lakini pia kuona namna unavyofanya kazi pale
ambapo watakutana nao.
‘’Tumepitisha mkataba
wa Paris wa kuungamkono juhudi za dunia katika kukabiliana na mabadiliko ya
tabia nchi hasa katika hewa ya ukaa hivyo ni muhimu kuwa na mfumo huo ambao
utatuwezesha Tanzania kujitathimini na kuona jitihada zinazofanyika pale
tunapotakiwa kutoa taarifa ya nchi kwenye umoja wa mataifa’’ Aliongeza Kitogo.
Amesema kupitia UNDP
wameweza kutafuta wataalamu hao na kuwapa kazi ya kutengeneza mfumo huo na
baada ya kuutengeneza sasa wameuleta na kuwafonyesha unavyofanya kazi na
kuwafundisha namna ya kuutumia maana ni mfumo ambao unabadilika hivyo unahitaji
kuboreshwa.
Kwa upande wake
mratibu wa kituo cha kitaifa cha kufuatilia hewa ya kaboni kilichopo SUA Prof.
Zahabu Eliakimu amesema kuwa mwanzoni wakati walipoanzsha kituo hicho cha
kitaifa walikuwa wamejikita kwenye kufuatilia hewa chafu zinazosababisha
mabadiliko ya tabia ya nchi walikuwa wanaiangalia zaidi hewa moja ya
kabondayoksidi lakini kupitia mfumo huu watahusisha hewa
zote saba zinazohusika katika kusababisha mabariliki ya tabia nchi.
Amezitaja hewa hizo
ambazo mfumo huu utahusika katika kuzifuatilia ukiachia mbali ile ya
carbondioxide ya awali ambazo zitaangaliwa katika kila sekta kuwa ni
Green house,Methane,Chlorofluorcarbon,Hydrofluorcarbon,Nitrous Oxide,Walter
Vapor pamoja na Ozone.
‘’Tunavyoenda na
kuzingalia hewa zote hizi tunabaki kuona kuwa hewa ambayo ndio inaongoza zaidi
katika kuchangaia mabadiliko hayo ya tabia ya nchi kuwa ni Carbondioxide lakini
hizo nyingine zinachangia kwa kiasi kidogo lakini sekta inayohusika zaidi ni
sekta ya matumizi ya ardhi kwenye mistu,kilimo makazi ya watu ndiyo
kupitia madaliko hayo’’ Alisema Prof. Eliakimu.
Kwa upande wake
Mataalamu mwandamizi wa mazingira kutoka ofisi ya makamu wa rais Bi.
Adelaida Tillya amesema kuwa mfumo huo ni muhimu sana kwa taifa kwani
utaisaidia nchi kuweka mikakati thabiti ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia
nchi kwakuwa sayansi imeonyesha vitu vinavyoweza kuachangia mabadiliko hayo na
namna ya kukabiliana nayo kama nchi na mtu mmojammoja.
‘’Tanzania inaonekana
haichangii kwa kiasi kikubwa katika mabadiliko ya tabia nchi kama ambavyo
zinachangia nchi zingine, lakini ni lazima kuangalia maendeleo ya nchi kama
tunapunguza au tunaongeza uzalishaji wa hewa ukaa’’ Alisema Bi. Tillya.
Ameongeza kuwa kwa
nchi zinazoendelea zimejiwekea mikakati ya kitaifa katika kuangalia
malengo ambayo nchi imejiwekea kama imefikiwa au la na kuweza kutoa ripoti kwa
mamlaka husika kila baada ya miaka miwili kama unavyotutaka Mkataba wa
kimataifa tuliousaini wa kuungana na nchi zingine duniani
katika kupunguza tatizo hili.
No comments:
Post a Comment