Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Prince Williams leo katika
Jumba la Kifalme la Buckingham Palace ikiwa sehemu ya ratiba zake jijini London
ambapo anamuwakilisha Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John
Pombe Magufuli katika mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali za Jumuiya za
Madola.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimbidhi picha ya kuchorwa Prince Williams
leo katika Jumba la Kifalme la Buckingham Palace kama zawadi na ishara ya
kutambua mchango wa Prince William katika kupambana na ujangili, Makamu wa Rais
yupo jijini London kumuwakilisha Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dk. John Pombe Magufuli katika mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali za
Jumuiya za Madola.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo
amekutana na kufanya mazungumzo na Prince William katika jumba la Kifalme la
Buckingham Palace.
Makamu wa Rais
alimweleza Prince William kuwa Tanzania inatambua mchango wake katika kuzuia
ujangili wa wanyama pori na Serikali ya Tanzania imekuwa ikichukua hatua mbali
mbali ya kupambana na kuzuia ujangili ingawa bado hatujawa na tekinolojia yenye
uwezo wa wa kutambua na kuona wanyama wote lakini tumeendelea kuimarisha ulinzi
wa wanyama pori.
Kwa upande wake Prince
Williams alimuahidi Makamu wa Rais kusaidia katika kuboresha ulinzi wa wanyama
pori kwa kutumia teknolojia ya hali ya juu na pia Prince William amemualika
Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika
mkutano unaohusu masuala ya Wanyapori unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka
huu jijini London.
Makamu wa Rais Mhe.
Samia yupo nchini Uingereza kumuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali
wa nchi za jumuiya ya Madola.
No comments:
Post a Comment