Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Januari Makamba
Akizungumza wakati wa
Kongamano lililofanyika mkoani Dodoma kuhusu Muungano lililowashirikisha
wanafunzi zaidi ya 300 wa vyuo vya elimu ya juu mkoani Dodoma Waziri wa Nchi
Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Januari Makamba amesema kuwa
vijana wanalo jukumu kubwa katika kulinda Muungano na kuudumisha.
“Vijana tunawategemea
muwe watetezi na walinzi wa Muungano wetu kwa kuwa huu ni urithi wa Taifa
tunawajibika kuulinda na kuudumisha kwa faida ya kizazi hiki na kijacho” Alisisitiza Makamba
Akifafanua Makamba
amesema kuwa vijna wanaowajibu wakuonesha uzalendo wao kwa kudumisha Muungano
ambao unalitambulisha taifa nje ya mipaka yetu.
Mambo mengine
yanayolitambulisha Taifa letu ni Lugha, Mipaka yetu, Historia, Utamaduni wa
kisiasa na kijamii.
“ Waasisi wa Taifa letu
walikuwa na dhamira njema ndio maana waliasisi Muungano wetu na kuweka mipaka
mipya ya Taifa letu tofauti na ile ya wakoloni hivyo hili ni jambo la
kujivunia” Alisisitiza Mhe. Makamba.
Aliongeza kuwa vijana
wanapaswa kuwapuuza wale wote wanaobeza Muungano kwa kuwa hawalitakii mema
taifa letu.
Kwa upande wake
mwanasiasa mkongwe na Waziri (mstaafu) wa baraza la kwanza la Mawaziri la
Serikali ya Awamu ya Kwanza mara baada ya Uhuru Balozi Job Lusinde akizungumza
katika mahojiano maalum mjini Dodoma amewaasa vijana kudumisha Muungano kwa
kujifunza historia ya Muungano ili waweze kushiriki kikamilifu katika kuuenzi.
“Vijana wajitahidi wawe
waadilifu kwa kulinda uhuru wetu, umoja wetu na muungano wetu kwa faida ya
kizazi hiki na kijacho” Alisisitiza Balozi Lusinde.
Akifafanua Balozi
Lusinde amesema vijana wanapaswa kuepuka vitendo vya wizi na ufisadi ili
kuchochea maendeleo.
Mada zilizotolewa katika
Kongamano hilo ni pamoja na Historia na faida za Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar, Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Mtazamo wa Kiuchumi, Kijamii na
Kisiasa.
Kongamano kuhusu
Muungano limefanyika Mkoani Dodoma ikiwa ni siku chache kabla ya maadhimisho ya
siku ya Muungano yanayotarajiwa kufanyika Aprili 26, 2018 mjini Dodoma, Kongamano
hilo limewahusisha wanafunzi wa Chuo Kikuu Dodoma, Mipango, CBE, St. John, Chuo
cha Madini na Chuo cha Maendeleo Vijijini Hombolo.
No comments:
Post a Comment