Serikali imetoa mchanganuo wa Tsh. Trilioni 1.5 zinazodaiwa kutojulikana
zilipo.
Akizungumza bungeni
leo Aprili 20, Naibu Waziri wa Fedha amesema kiasi cha Sh697 bilioni kilitumika
katika matumizi ya dhamana na hati fungani zilizoiva, Sh 687bilioni kwa ajili
ya mapato tarajiwa na Sh 203 bilioni ni za mapato ya kodi yaliyokusanywa kwa niaba
ya Serikali ya Zanzibar.
Naibu Spika amesema
bungeni hapo, maswali na majibu yatapangiwa utaratibu mwingine.
“Hakuna Fedha kiasi
cha Sh1.5trilioni iliyopotea au kutumika kwenye matumizi ambayo
hayakuidhinishwa na Bunge tukufu. Madai ya watu wasiyoitakia mema nchi kuhusu
matumizi ya fedha hii hawana nia njema na nchi,” amesema Dk Kijaji
Amesema kutoonekana
kwa fedha hiyo kulitokana na taarifa ya ukaguzi ya CAG kutumia taarifa za
hesabu za nyaraka mbalimbali na hivyo kutojumuishwa kwa baadhi ya taarifa za
utekelezaji wa bajeti.
Amesema hadi kufikia
Juni 2017, mapato yalikuwa Sh 25.3 trilioni na matumizi yalikuwa Sh23.79
trilioni.
“Matumizi haya hayakujumuisha Sh
697.85bilioni zilizotumika kulipa dhamana na hati fungani za serikali
zilizoiva,” amesema
Hivi karibuni,
Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, alizungumza na vyombo vya
habari na kueleza kuwa katika ukurasa wa 34 wa ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti
Mkuu wa Hesabu za serikali, (CAG)Sh 1.5 trilioni hazikutolewa kwa matumizi wala
kukaguliwa.
No comments:
Post a Comment