Waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye amemtangaza Bw.Hassan Abbas kuwa Mkurugenzi wa Idara ya
Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa
Serikali kuanzia Agosti 5 Mwaka huu.
Uteuzi huo umefanyika
kwa mujibu wa Sheria za Utumishi wa Umma Namba 8 ya mwaka 2002 kifungu Namba
6(1)(b) kufuatia uhamisho wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara hiyo Bw. Assah
Mwambene uliofanyika tarehe 7 Machi 2016
kwenda Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Mhe.Nape Moses Nnauye ametoa wito kwa Wanahabari
na Wananchi kwa ujumla kutoa ushirikiano
wa kutosha kwa Bw Abbas atakapokuwa anatekeleza majukumu yake.
“Ninawaomba
Wanahabari na Watanzania kwa ujumla mumtambue Bw Abbas na mtoe ushirikiano
unaostahili katika utendaji wa kazi zake”.Alisema Mhe. Waziri.
Aidha Mhe.
Waziri Nape alimpongeza Bibi Zamaradi Kawawa aliyekuwa anakaimu nafasi hiyo kwa
kujituma na kusimamia majukumu yote ya
Idara kwa ukamilifu na uadilifu.
Kwa upande wake
Mkurugenzi huyo mpya amekubali uteuzi huo na ameahidi kuitumikia nafasi hiyo
kwa uadilifu mkubwa na ameomba ushirikiano wa kutosha kutoka kwa wafanyakazi wa
Idara ya Habari Maelezo na Watanzania kwa ujumla.
Kabla ya uteuzi
huo Bw. Hassan Abbas alikuwa ni Meneja
Habari na Mawasiliano katika Ofisi ya Rais inayosimamia Utekelezaji wa Program
ya Matokeo Makubwa sasa (President`s Delivery Bureau).
No comments:
Post a Comment