Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa.
Waziri Mkuu wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amesema kwamba Tanzania haitapata
upungufu wa sukari kutokana na kuanza kwa uzalishaji wa sukari kwa viwanda vya
ndani.
Waziri Mkuu ameyasema
hayo leo Bungeni, Mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge Suleiman
Ahmed Sadick alipotaka ufafanunuzi namna ambavyo Serikali ya Awamu
ya Tano imejipanga ikiwa tatizo la upungufu wa sukari litajirudia tena.
“Tayari Viwanda vya ndani vimeanza
uzalishaji wa sukari ambapo kufikia mwisho wa mwezi Machi mwaka huu ambao ndio
mwisho wa msimu tutakuwa tumefikia lengo la uzalishaji wa sukari kwa nchi
nzima,” alifafanua Majaliwa.
Aidha, Waziri Mkuu
amewataka wafanyabiashara kutoweka vyakula ndani ili kuviuza kwa bei ya juu
baadae, badala yake amewataka kuuza vyakula hivyo ili kuongeza upatikanaji wa
chakula nchini, kwani uongezaji wa bei wa vyakula unaumiza wananchi wa kipato
cha chini na kati.
Katika
kukabiliana na tatizo la ukame kwa baadhi ya maeneo hapa nchini, Waziri Mkuu
amewataka wakulima kutumia kipindi hiki ambacho baadhi ya maeneo yanapata mvua
kwa kupanda mazao ya muda mfupi ambayo pia mazao hayo yataweza kutumika kwa
msimu ujayo.
No comments:
Post a Comment