Mjumbe wa halmashauri kuu ya Taifa ya chama cha mapinduzi(CCM) Mkoani
Geita Iddi Kassim Iddi,amefanikisha upatikanaji wa kiasi cha shilingi milioni
13.2 ,mifuko ya seruji 70 na mabanti ya kisasa 131 kwaajili ya ujenzi wa
madarasa ya watoto kwenye kanisa la AIC Kalangalala Wilayani Geita.
MNEC wa mkoa huo Iddi ameendesha harambee hiyo siku ya jana kwenye ibada
ambayo ilikuwa imeandaliwa na idara ya wanawake wa kanisa la AIC
Kalangalala kwaajili ya changizo la umaliziaji wa madarasa ya kujifunzia watoto
kanisani hapo.
Akisoma risala mbele ya mgeni rasmi kwa niaba ya watoto wa kanisa
hilo,Bi Justina Yuda ameeleza mahitaji ya ujenzi wa madarasa ya watoto
kwa awamu ya pili yanatarajia kugharimu kiasi cha Tsh 19,185,000 na
kwamba fedha hiyo itasaidia kuezeka,kuweka dali kwenye madarasa pamoja na
kuweka frame za madirisha ,milango na mageti ya milango.
Katika harambee hiyo MNEC Iddi milioni 1 papo hapo,mifuko 20 ya seruji na
mabati 13 huku akitumia nafasi hiyo kuendesha harambee ambayo iliweza kusaidia
kupatikana kiasi cha sh,milioni 12.2 hivyo kupelekea kupatikana kwa jumla ya
kiasi cha sh,milioni 13.2 ambazo zitatumika kujenga madarasa ya kujifunzi
watoto.
Akihutubia mamia ya waumini hao Mara baada ya kupewa nafasi ya
kuwasalimia waumini wa kanisa hilo MNEC Iddi aliwasisitiza waumini hao
kuendelea kuunga jitihada za uchangiaji wa madarasa pamoja na ujenzi hili
kuweza kutatua changamoto ambayo imeendelea kuwakabili wanafunzi wengi kwa
sasa.
Pia amewaomba kundelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali
ya awamu ya inayooongozwa na kusimamiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano Wa
Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kwani imejipambanua kuwanufaisha wananchi
kupitia rasilimali zao.
Aliwasihi waumini hao kuiombea serikali ya Rais Magufuli sambamba na
wateule na watumishi wake wote ili waendelee kuliongoza Taifa na sekta
mbalimbali katika ushirika mwema wakiongozwa na roho mtakatifu kila mmoja kwa
imani yake.
Aidha kwa upande wake mchungaji wa kanisa hilo John Masanyiwa alisema
kukamilika kwa madarasa hayo matatu yatawasaidia watoto kuweza kujifunza
katika vipindi vya ibada na pia kwa upande wa idara ya wanawake yatawasaidia
kuwa kama kitega uchumi kwa maana ya kukodisha kwaajili ya shughuli mbali mbali
zikiwemo za semina na warsha ambazo zitakuwa zikifanyika.
Pia,Mch Masanyiwa amemshukuru MNEC wa mkoa wa Geita kwa kufanikisha
shughuli ya harambee hiyo.
No comments:
Post a Comment