Monday 26 March 2018

WAWEKEZAJI WAZAWA WAPEWA RAI KUJENGA VIWANDA VYA DAWA



Rais Dkt. John Pombe Magufuli akibadilishana mawazo na Mwakilishi wa Global Fund Linden Morrison wakati wa hafla ya kukabidhi magari 181 yatakayokuwa yakisafirisha vifaa tiba na vitendanishi katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini. Hafla hiyo ilifanyika leo Jumatatu Machi 26, 2018 katika Ofisi za MSD Keko Mwanga Jijini Dar es Salaam.



Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiteta jambo na Waziri wa wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati wa hafla ya kukabidhi magari 181 yatakayokuwa yakisafirisha vifaa tiba na vitendanishi katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini. Hafla hiyo ilifanyika leo Jumatatu Machi 26, 2018 katika Ofisi za MSD Keko Mwanga Jijini Dar es Salaam.



Mkurugenzi Mkuu wa Bohari Kuu ya Madawa, Laurean Bwanakunu akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi magari 181 yatakayokuwa yakisafirisha vifaa tiba na vitendanishi katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini. Hafla hiyo ilifanyika leo Jumatatu Machi 26, 2018 katika Ofisi za MSD Keko Mwanga Jijini Dar es Salaam.




Mkurugenzi Mkuu wa Bohari Kuu ya Madawa, Laurean Bwanakunu akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi magari 181 yatakayokuwa yakisafirisha vifaa tiba na vitendanishi katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini. Hafla hiyo ilifanyika leo Jumatatu Machi 26, 2018 katika Ofisi za MSD Keko Mwanga Jijini Dar es Salaam.




Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi magari 181 yatakayokuwa yakisafirisha vifaa tiba na vitendanishi katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini. Hafla hiyo ilifanyika leo Jumatatu Machi 26, 2018 katika Ofisi za MSD Keko Mwanga Jijini Dar es Salaam



Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi magari 181 yatakayokuwa yakisafirisha vifaa tiba na vitendanishi katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini. Hafla hiyo ilifanyika leo Jumatatu Machi 26, 2018 katika Ofisi za MSD Keko Mwanga Jijini Dar es Salaam.



Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda  wakati wa hafla ya kukabidhi magari 181 yatakayokuwa yakisafirisha vifaa tiba na vitendanishi katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini. Hafla hiyo ilifanyika leo Jumatatu Machi 26, 2018 katika Ofisi za MSD Keko Mwanga Jijini Dar es Salaam.




Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza wakati wa hafla ya  magari 181 yatakayokuwa yatayosafirisha vifaa tiba na vitendanishi katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini. Hafla hiyo ilifanyika leo Jumatatu Machi 26, 2018 katika Ofisi za MSD Keko Mwanga Jijini Dar es Salaam.



Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza wakati wa hafla ya  magari 181 yatakayokuwa yatayosafirisha vifaa tiba na vitendanishi katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini. Hafla hiyo ilifanyika leo Jumatatu Machi 26, 2018 katika Ofisi za MSD Keko Mwanga Jijini Dar es Salaam



Rais Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria uzinduzi wa magari 181 yatakayokuwa yatayosafirisha vifaa tiba na vitendanishi katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini. Hafla hiyo ilifanyika leo Jumatatu Machi 26, 2018 katika Ofisi za MSD Keko Mwanga Jijini Dar es Salaam



Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,. Jinsia, Wazee na Watoto akibadilishana mawazo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wakati wa hafla ya kukabidhi magari 181 yatakayokuwa yakisafirisha vifaa tiba na vitendanishi katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini. Hafla hiyo ilifanyika leo Jumatatu Machi 26, 2018 katika Ofisi za MSD Keko Mwanga Jijini Dar es Salaam.



Rais Dkt. John Pombe Magufuli akishuka katika moja ya magari 181 yatakayokuwa yakisafirisha vifaa tiba na vitendanishi katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini. Hafla hiyo ilifanyika leo Jumatatu Machi 26, 2018 katika Ofisi za MSD Keko Mwanga Jijini Dar es Salaam.



Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mwakilishi wa Global Fund na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakati wa hafla ya kukabidhi magari 181 yatakayokuwa yakisafirisha vifa tiba na vitendanishi katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini. Hafla hiyo ilifanyika leo Jumatatu Machi 26, 2018 katika Ofisi za MSD Keko Mwanga Jijini Dar es Salaam.



Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Mwakilishi Mkazi wa Global Fund, Linden Morrison wakifurahia jambo na wafanyakazi wa Bohari Kuu ya Madawa (MSD) mara baada ya kukabidhi magari 181 yatakayokuwa yakisafirisha vifa tiba na vitendanishi katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini. Hafla hiyo ilifanyika leo Jumatatu Machi 26, 2018 katika Ofisi za MSD Keko Mwanga Jijini Dar es Salaam.




Rais Dkt. John Pombe Magufuli akikagua baadhi ya magari 181 yatakayokuwa yakisafirisha vifa tiba na vitendanishi katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini. Hafla hiyo ilifanyika leo Jumatatu Machi 26, 2018 katika Ofisi za MSD Keko Mwanga Jijini Dar es Salaam



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametoa rai kwa wawekezaji wazawa na wafanyabiashara nchini kujenga viwanda vya dawa na vifaa vya tiba hapa nchini ili kuongeza kasi ya ujenzi wa uchumi wa viwanda na kukuza ajira.

Rais Magufuli ametoa rai hiyo leo Jijini Dar es Salaam, kwenye hafla ya uzinduzi wa magari 181 yenye thamani ya shilingi bilioni 20.7 ya kusambaza dawa na vifaa vya tiba yaliyotolewa msaada na Shirika la Global Fund kwa Serikali ya Tanzania kupitia Bohari ya Dawa (MSD).

“Asilimia 94 ya dawa zinanunuliwa nje ya nchi, hivyo wawekezaji wazawa watumie changamoto hii kama fursa ya kuanzisha viwanda vya dawa na vifaa tiba hapa hapa nchini kwetu,” alisema Rais Magufuli.

Rais Magufuli alibainisha kuwa ujenzi wa viwanda hapa nchini utasaidia kuongeza ajira kwa Watanzania hasa vijana pamoja na kupunguza gharama za kuagiza bidhaa nje ya nchi zikiwemo dawa na vifaa vya tiba.

Aidha Rais Magufuli ametoa wito kwa wataalamu na wasomi wazawa wa masuala ya afya na tiba kujiunga pamoja na kuanzisha viwanda vya dawa ili kuchochea uchumi wa viwanda na kuongeza mapato.
“Tunapoteza shilingi bilioni 500 kila mwaka kwa ajili ya kununua dawa nje ya nchi lakini tungekuwa na viwanda vyetu fedha hizo tungetumia kwenye mambo mengine ya maendeleo,” alisisitiza Rais Magufuli.

Pia Rais Magufuli alisisitiza kuwa madereva watakaoajiriwa kuendesha magari hayo mapya wachaguliwe kwa umakini ili kupata watu waaminifu watakaoweza kuyatunza kwa manufaa ya Watanzania.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa Tanzania (MSD) Bw. Laurian Bwanakunu ameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli kwa kuongeza bajeti ya ununuzi wa dawa kutoka bilioni 31 mwaka 2015/2016 hadi kufikia bilioni 269 mwaka 2017/2018.

Pia Bwanakunu amewashukuru Global Fund kwa msaada huo wa magari ambayo yataongeza kasi ya usambazaji wa dawa nchi nzima kila baada ya miezi miwili.

Bohari ya Dawa Tanzania (MSD) ilianzishwa mwaka 1994 kwa ajili ya kununua, kuhifadhi na kusambaza dawa na vifaa vya tiba nchini kote.



No comments:

Post a Comment