Mbunge wa Jimbo la Nyang'hwale Mhe Hussein Nassor Amari Kasu akizungumza na kuelezea kero ambazo wamekuwa wakizipata wachimbaji wadogo za kuondolewa kila mala kwenye maeneo ambayo wanayazindua. |
Mkuu wa wilaya ya Nyang'hwale Hamim Gweyama akiwaeleza wachimbaji kufuata taratibu na sheria ambazo zimewekwa kwenye maeneo ya uchimbaji madini. |
Serikali imesema imedhamiria kuwanufaisha wananchi kupitia rasilimali za
nchi hususani sekta ya Madini hivyo wachimbaji wadogo wanapaswa kuzingatia
maelekezo ya serikali ikiwemo taratibu na sheria katika uchimbaji.
Naibu Waziri wa Madini Bw DotoBiteko ametoa kauli hiyo wakati akizungumza
na wachimbaji wadogo katika Kijiji cha Bululu, kilichopo Kata ya Nyamtukuza
Wilayani Nyang'hwale Mkoani Geita.
Alisema Serikali imetenga maeneo maalum kwa wachimbaji wadogo katika mkoa
wa Geita na maeneo mengi nchini huku akisisitiza kuwa kuna leseni za utafiti na
uchimbaji mdogo 24 ambazo zinaisha muda wake March 30 mwaka huu katika Wilaya
ya Nyang'hwale.
Amewataka wananchi kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kwa kuwa Serikali inatazama
namna ya kuwapatia wachimbaji wadogo baadhi ya maeneo hayo.
Naibu waziri Biteko ameendelea kusema kuwa serikali itatoa
leseni kwa ajili ya maeneo ya uchimbaji lakini haitatoa leseni hizo kwa mtu
mmoja mmoja badala yake amewasihi wachimbaji hao kuanzisha vikundi ili kupatiwa
leseni hizo.
Mbunge wa Jimbo la Nyang’hwale Bw Hussein Kasu alimueleza Naibu
waziri kuwepo kwa tabia ya kufukuzwa wachimbaji wadogo
hata kama wanakuwa wakivumbua maeneo ambayo yanadhahau kwa madai kuwa yapo
ndani ya leseni hali ambayo imewapelekea kujiona kama wao ni wakimbizi.
Hata hivyo kufuatia agizo ambalo limetolewa na Naibu waziri wa madini Bw
Biteko, baadhi ya wachimbaji wamesema matarajio yao yalikuwa ni kuruhusiwa
kuendelea kufanya kazi kwenye maeneo ambayo walikuwa
wameanza uchimbaji hivyo hawaafiki kuendelea kusubilia hadi tarehe
ambayo wameambiwa .
Aidha Biteko pia amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Nyang'wwale Bw
Hamim Gwiyama kuitisha kikao ndani ya wiki moja kwa kuwaalika wananchi wote
wenyewe vikundi ili kuwaelekeza namna bora ya kufanya kazi za uchimbaji kwa
kufuata taratibu na sheria.
No comments:
Post a Comment