Halmashauri nchini zimetakiwa kuhakikisha zinaanzisha mifuko ya
dawa na vifaa tiba ili kurahisisha upatikanaji wa huduma katika Hospitali,
Vituo vya Afya na Zahanati katika maeneo yao.
Agizo hilo limetolewa jana, Mei 2 na Rais Dkt. John Pombe
Magufuli katika hafla ya kuweka jiwe la msingi la Hospitali ya Wilaya ya
Kilolo, mkoani Iringa.
Rais Magufuli alisema kuwa kuanzishwa kwa mifuko hiyo kutasaidia
upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kwa urahisi kwakuwa halmashauri zitakuwa na
uwezo wa kununua moja kwa moja kupitia fedha zitakazotokana na mifuko hiyo.
“Natumia fursa hii kuziagiza Halmashauri zote nchini kuanzisha
mifuko ya dawa na vifaa tiba (Drug Funds), hili isaidie katika kurahisha
upatikanaji wa dawa na vifaa tiba katika maeneo yenu”, Alisisitiza Rais
Dkt. Magufuli.
Aliongeza kuwa katika kutambua umuhimu wa upatikanaji wa dawa na
vifaa tiba Serikali imetenga Sh.50 Bilioni katika bajeti yake ya mwaka wa fedha
2018/19.
No comments:
Post a Comment