Mkufunzi wa kilabu ya Manchester United Louis van Gaal amefutwa
kazi kama mkufunzi wa klabu ya Manchester United ,huku aliyekuwa mkufunzi wa
Chelsea Jose Mourinho akitarajiwa kuchukua mahala pake.Raia huyo wa Uholanzi
anaondoka baada ya kukamilisha miaka miwili ya kandarasi yake kati ya
mitatu.Kitengo cha habari za michezo cha BBC Sport kiliripoti siku ya Jumamosi
kwamba ushindi wa United wa kombe la FA dhidi ya Crystal palace utakuwa mechi
yake ya mwisho akiwa mkufunzi.Uteuzi wa Mourinho unatarajiwa kuthibitishwa
baada ya raia huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 53 kukutana na maafisa wakuu
wa United siku ya Jumanne.
No comments:
Post a Comment