Monday 20 March 2017

MTOTO AKAMATWA NA NOTI BANDIA YA ELFU KUMI MKOANI GEITA



Mtoto wenye umri wa miaka 11 anaetambulika kwa jina la Emmanuel Metusela mkazi wa mji mdogo wa Katoro wilayani na mkoani Geita ameshikiliwa na jeshi la jadi (sungusungu) kwa kukutwa na noti bandia shilingi elfu kumi.
Tukio hilo limetokea  jana mtaa wa stooni  katika mamlaka ya mji mdogo wa katoro ambapo mtoto huyo amekamatwa na noti bandia pindi alipo kuwa akijaribu kwenda kununua vocha katika duka lililopo mtaani hapo.

Akizungumza mtoto huyo amesema kuwa hela hiyo alipewa na mtu ambae hamfahamu akamchukulie vocha dukani pasipo kujua kama ni noti bandia ndipo alipo kamatwa na mwenye duka na kuambiwa kuwa noti hiyo ni bandia.

Kwa upande wake Bw.Moses Nganikie mmiliki wa duka ambalo tukio hilo limetokea amesema kuwa kijana huyo alikuja mara ya kwanza akiwa na noti ya elfu kumi akanunua vocha ya elfu moja kisha akaondoka baada ya kijana yule kuondoka  ndipo alipo chukua noti ile ya shilingi elfu kumi kwa lengo la kuchukua sigara kwa jirani yake ndipo walipo gundua kuwa noti ile ni bandia baada ya muda mfupi mtoto yule akarudi tena na noti nyingine ndipo walipo shituka na kumkamata.


Aidha  kamanda mkuu wa jeshi la jadi (sungusungu) wa mtaa huo Bw. Marchades Gervas alithibitishwa  kukamatwa kwa mtoto huyo ambapo uchunguzi zaidi unaendelea kubaini kiini cha tukio hilo.

No comments:

Post a Comment