Mbunge wa jimbo la Geita mjini,Constatine Kanyasu akizungumza na wananchi wa mtaa wa msalala road kata ya kalangalala wakati wa mkutano wa kusikiliza kero za wananchi. |
Mbunge wa jimbo la Geita mjini,Constatine Kanyasu akifurahia pamoja na wakina mama ambao walikuwa wakiimba kwenye mkutano huo. |
Katibu wa itikadi na uenezi wa chama cha mapinduzi(CCM)Kata ya kalangalala,Richard Nzagamba akizungumza na wananchi wakati wa mkutano wa mbunge wa jimbo la Geita mjini. |
Mwenyekiti wa mtaa wa Msalala road,Sostenes Calist Idory akielezea kero za ubovu wa mabarabara kwenye mtaa mbele ya Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini. |
Katibu wa UVCCM Wilaya ya Geita,Ally Rajabu akielezea namna ambavyo waendesha Baiskeli walivyoondolewa katikati ya mji kufanya shughuli zao za kila siku. |
Diwani wa kata ya Kalangalala ,Sospeter Mahushi akifurahia na wananchi wakati wa mkutano wa mbunge wa jimbo la Geita mjini. |
Diwani wa kata ya Kalangalala ,Sospeter Mahushi akizungumza na wananchi wakati wa mkutano wa mbunge wa jimbo la Geita mjini ambao ulikuwa na lengo la kusikiliza kero za wananchi. |
Mbunge wa jimbo la Geita mjini Constantine Kanyasu, amepinga tamko la
mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya mji wa Geita Mhandisi Modest
Apolinary alilolitoa hivi karibuni akiwataka wasafirishaji wa
abiria kwa kutumia Baiskeli maarufu kwa jina la Daladala kusitisha shughuli
hizo mjini Geita kwa madai kuwa wamekuwa chanzo cha ajali mjini humo.
Bw. Kanyasu akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wakati akisikiliza na
kujibu kero za wananchi wa mtaa wa Barabara ya Msalala Kata ya Kalangalala
alisema kuwa muda wa kuwazuia waendesha baiskeli kutoa huduma hiyo haujafika
bali waendelee kufanya kazi bila kubughudhiwa .
Alisema kuwa aliyetoa tamko la kuwazuia waendesha Baiskeli hao kwa madai
kuwa wanasababisha ajali mjini hakufanya utafiti na kwamba hakuna kikao
cha Baraza la madiwani kilichoketi na kukubaliana kuwa waendesha baiskeli hao
maarufu Daladala wasitishe kutoa huduma hiyo mjini hivyo wataendelea kutoa
huduma ya kubeba abiria kama kawaida.
Bw Kanyasu alisema kuwa mji wa Geita unakuwa lakini yeye
binafisi amefanikiwa kufika China licha ya kupiga hatua kubwa kimaendeleo
pamoja na teknolojia wananchi wa Taifa hilo bado kwenye barabara zao
wanaendesha baiskeli hivyo bajaji na Pikpiki maarufu kama bodaboda pamoja na
daladala waendele kufanya kazi kwa kufuata sheria za barabarani kwa kuwa
wote wana haki ya kutafuta riziki kwa kutumia kazi zao.
''Waendesha daladala za baikeli, Bajaji
na waendesha Pikipiki wote wana haki ya kufanya kazi, aliyetoa tamko la kuzuia
baiskeli hakufanya utafiti kwanza na hakuna kikao chochote walichokaa madiwani
wakakubalina, hivyo muda ukifika watajiondoa wenyewe ", alisema Kanyasu .
Aidha katibu wa umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi, UVCCM wilayani
Geita Bw Rajab Ally Rajab akitoa salaam za chama hicho kwenye mkutano huo
alipinga hatua ya mkurugenzi huyo na kusema kuwa serikali haiwezi kuwazuia
waendesha Baiskeli hao kutoa huduma hiyo mjini bila kuwaandalia mazingira ya
eneo la kutolea huduma hiyo na kwamba chama hicho hakiko tayari kuona vijana
wanahangaika .
"Wanaofanya kazi ya kuendesha daladala za
baiskeli wengi ni vijana na ni wapiga kura wa chama change, Chama
hakiwezi kukubali watimuliwe mjini watafanyia kazi zao wapi bila
kuwaandalia mazingira? Mkurugenzi hakukishirikisha chama tulishituka baada ya
kusikia matangazo", alisema katibu Ally
Rajabu.
Hivi karibuni mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya mji wa Geita
aliwatangazia waendesha daladala za baiskeli kusitisha kutoa huduma ya kubeba
abiria mjini na badali yake wafanye shughuli zao kwenye maeneo ambayo walikuwa
wamepangiwa yakiwemo ya Nyankumbu na Mwatulole pembezoni mwa mji
kwa madai kuwa wamekuwa chanzo cha ajali za barabarani mjini hali
iliyosababisha kuibua maandamano makubwa ya waendesha daladala hadi
katika ofisi za mbunge wa jimbo la Geita mjini .
No comments:
Post a Comment