Leo June 20 2016 baadhi ya magazeti yameibuka
na taarifa ambazo imedai kuwa mafuta ya taa yameadimika katika mikoa kadhaa
nchini ikiwamo Dar es salaam, Morogoro, Mwanza, Mtwara na Mikoa ya Kanda ya
Kaskazini.
Mkurugenzi wa mafuta ya Petrol
kutoka mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na Maji(EWURA) injinia Godwin Samweli amekanusha taarifa hizo na
kusema hakuna upungufu wa mafuta ya taa nchini kwa sababu yapo ya
kutosha na meli kubwa imemaliza kushusha lita milioni 2.5 ambazo zitatumika kwa
siku 20 na mengine yapo kwenye matanki.
tuna mafuta mengi tu, mengine
yameshuka leo na mengine yako kwenye matanki, kila mwezi lazima kuna shehena ya
mafuta ya taa inakuja, kwa siku moja kwa matumizi yetu ni kama lita
126,000‘
’hakuna mfanyabiashara atakuwa na pampu ya
mafuta ya taa halafu akatae kuuza mafuta ya taa, kama kuna mkoa mmoja au miwili
ambayo imetokea hivyo huenda gari limeharibika njiani, lakini wafanyabiashara
wako makini sana kufanya biashara, kama mafuta yapo hapa Dar es salaam ni
lazima watayapeleka kwenye vituoa vyao‘
No comments:
Post a Comment