Italy leo wanawania
ushindi wa pili ili kujihakikishia nafasi ya kufuzu hatua ya 16 bora ya
michuano ya Euro pale watakapokuwa na kibarua kigumu mbele ya Sweden, katika
mchezo wa kundi E utakaofanyika kwenye uwanja wa Stade de Toulouse uliopo
manispaa ya manispaa ya Tolouse majira ya saa 10 jioni.
Italy maarufu kama
Azzurri walionesha ukomavu wake katika mchezo wa awali uliochezwa Jumatatu
dhidi ya Ubelgiji baada ya kushinda mabao 2-0, magoli yaliyofungwa na Emanuele
Giaccherini na Graziano Pelle licha ya muda mwingi kuelemewa na wapinzani wao.
Ushindi wa leo
utawafanya vijana hao wa Antonio Conte kufuzu moja kwa moja hatua ya mtoano na
kuwasubiri wapinzani wao wengine watakaokuwa wakiwania nafasi ya kuungana nao.
“Nadhani nina kundi la
wachezaji wenye akili nyingi mno katika kikosi changu, wengi wao wana hamu ya
kuona tunafanya kitu chenye tija, na ndio maana tunapambana kuhakikisha
tunavuka hatua hii ya makundi.” amesema Conte.
“Wanafahamu fika
kwamba, tunapaswa kupambana kwa asilimia 100, kwasababu kama tuncheza kwa
kiwango cha kawaida, tafsiri yake hatuwezi kupata matokeo. Ni lazima tufanye
kitu cha ziad ili kuwafanya mashabiki wetu wajivunie timu yao.”
Kwa upande wa Sweden
walianza kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Jamhuri ya Ireland, walipata goli dakika
ya 71, goli ambalo Jamhuri ya Ireland walijifunga wenyewe.
Macho yote kwa siku ya
leo tena yatakuwa kwa nahodha wa Sweden Zlatan Ibrahimovic ambaya anasaka kuwa
mchezaji wa kwanza kufunga kwenye michuano minne mfululizo ya Ulaya na kumzidi
Cristiano Ronaldo baada ya kushindwa kuonesha uwezo wake kwenye mchezo wa
kwanza.
Lakini kocha wa Sweden
Erik Hamren amemtetea nahodha wake huyo na kuwaasa wachezaji wake wote kwa
umoja wao kucheza kwa badii kuhakikisha wanapata matokeo ya ushindi.
“Ili kuwa mshambuliaji
bora, lazima upata sapoti kwa wachezaji wenzako. Safu yetu ya ushambuliaji
haikuwa katika ubora unaohitajika. Ndani ya dakika 50 za mwanzo washambuliaji
wetu hawakuwa wakipewa huduma nzuri.”amesema Hamren
“Tulianza kuingia
mchezoni taratibu na kuanza kutengeneza nafasi. Ibrahimovic alihusika kwenye
lile goli. Tunatakiwa kujitolea kwa asilimia 300 kwenye mechi zijazo kama
tunataka kushinda.”
Takwimu muhimu
kuelekea mchezo wa leo
Italy
Magoli saba kati ya tisa ya mwisho ya Italy
dhidi ya Sweden yamefungwa katika kipindi cha kwanza.
Chini ya Antonio Conte, Italy hawajafungwa
mechi 11 za ushindani (ushindi mara 8, droo tatu). Kipigo chao cha mwisho
kilikuwa dhidi ya Uruguay wakati wa fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014
(wakati huo ikiwa chini ya Cesare Prandelli)
Katika michezo ya mwisho 34 ya michuano ya
Ulaya, Italy hawajafunga zaidi ya magoli mawili.
Katika michezo yao 3 ya mwisho, Italy wamecha
bila kuruhusu nyavu zao kutikiswa.
Italy wamepoteza michezo miwili tu kati ya 22
katika hatua ya makundi ya fanali za michuano ya Ulaya (wameshinda mara 11,
sare mara 9)
Antonio Candreva amehusika katika magoli
matatu katika michezo miwili iliyopita kwa Italy (amefunga goli moja na kutoa
assist mbili)
Sweden
Sweden wameshinda michezo yao mitatu tu kati
ya 15 katika michuano ya Ulaya (sare 5 na kufungwa mara saba).
Licha ya kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Jamhuri
ya Ireland, Sweden hawakupiga hata shuti moja lililolenga lango.
Zlatan Ibrahimovic anaweza kuwa mchezaji wa
kwanza kufunga mara nne katika michuano minne tofauti ya Ulaya kama atafunga
leo. Mpaka sasa ana magoli sita katika michezo 11, ukijumlisha na ule dhidi ya
Italy mwaka 2004.
Magoli saba ya mwisho ya Sweden yamefungwa na
wachezaji saba tofauti (liliwemo moja la kujifunga).
No comments:
Post a Comment