Jeneza lililobeba mwili wa marehemu Valence Robart Mulamula ukiwa nje ya nyumba yao kwaajili ya heshima ya mwisho kabla ya kwenda kuzikwa kwenye makazi yake ya milele. |
Baba wa Marehemu wa katika kati akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi ambaye alifika kutoa pole na kushiriki mazishi. |
Mkuu wa wilaya ya Geita akitoa pole kwa mama wa Marehemu Valence Robart. |
Mkuu wa wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi (katikati)akibadirishana mawazo na Mwenyekiti wa halmashauri ua mji wa Geita pamoja na mwakilishi wa wafanyabiashara Mkoani Geita. |
Mwili wa Marehemu Valence Robart ukitolewa Nje. |
Mkuu wa wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi ,akitoa heshima za mwisho kwenye mwili wa marehemu Valence Robart. |
Mwenyekiti wa halmashauri ya Mji Lernad Kiganga Bugomola akitoa heshima za mwisho na kuuaga mwili wa mwanahabari Valence Robart. |
Mwakilishi wa wafanyabiashara Mkoani Geita,Saimon akiaga mwili. |
Mwandishi wa ITV Mkoani Geita,Rose Mweko akitoaga mwili wa marehemu Valence Robart. |
Marehemu Valence Robert alianza
kusumbuliwa na maradhi mwaka jana mwishoni na katika juhudi za kutafuta
matibabu alipelekwa jijini mwanza ambapo alipatiwa matibabu na kurudia
hali yake ya awali na kuendelea na Majukumu yake ya kazi lakini Mwanzoni mwa
mwaka huu mwezi wa pili hali yake ya afya ilibadirika na kupelekea kuzidiwa
mwezi wa tatu hali ambayo ilimrazimu kurudi Nyumbani kwaajili ya matibabu.
Kwa Mujibu wa Mzazi wake wa Kiume
,Mzee Robert Mulamula alisema kuwa hali yake ilibadirika ghafra siku ya juma
nne ya tarehe 28 na walipo kuwa katika jitihada za kutaka kumkimbiza hospitali
hali ilibadirika na kupelekea kukata kauli .
Mkuu wa Wilaya ya Geita Mwilimu
Herman Kapufi amewataka wazazi kuwa na Moyo wa subira na kuachana na dhana
ambazo zimekuwa zikiibuka pindi mtu anapofariki kuwa amelogwa na kwamba jambo
hilo sio la kweli kwani marehemu alikuwa ni mgonjwa kama ambavyo wengine
wamekuwa wakiugua.
Akimwakilisha Mbunge wa viti
maalum kwa Tiketi ya chama cha demokrasia na maendeleo Mkoani Geita Upendo
Peneza katibu wake Shida Mpondi alisema kuwa mbunge huyo ameupokea msiba
huo kwa masikitiko makubwa kwani marehemu Valence Robart alikuwa ni mtu wa
karibu ambaye walikuwa wakishirikiana katika kazi za ujenzi wa Taifa.
Hata Hivyo Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Mji wa Geita,Leornad Bugomola ,aliwaasa wanajamii ,ndugu na
jamaa wa karibu wa marehemu kuendelea kujikabidhi mikononi mwa Mungu kwani
hayupo hajuae siku wala saa ya kuondoka Duniani.
Marehemu Valence Robart
wakati wa uhai wake ameshawai kuwa mwandishi wa habari wa Channel Ten na gazeti
la Tanzania daima Mkoani Geita.
Na alizaliwa Tarehe 9mwezi wa 11
mwaka 1986 katika kijiji cha Mugana Wilayani Misenyi Mkoani Kagera akiwa ni
mtoto wa kwanza kwenye familia ya mzee Robart Mulamula na alifariki tarehe 28
mwezi wa 3 mwaka 2017.
No comments:
Post a Comment