Mkuu wa Wilaya ya Geita Ambaye ndiye alikuwa
mgeni Rasmi Mwl Herman Kapufi akielezea juu ya misingi na uhuru wa kuabudu.
Ayoub Bwanamadi akisoma Risala mbele ya mgeni
Rasmi.
Sheikh Mkuu wa Mkoa huo,Alhaji Yusufu
Kabaju akielezea kusikitishwa kwake na taarifa za watumishi kufanya kazi siku
kuu ya idd.
Baraza la waislamu (BAKWATA) Mkoani Geita limesikitishwa na kitendo
ambacho kimeendelea cha baadhi ya watumishi wa kwenye
Halmashauri ya Wilaya ya Geita kufanyiwa zoezi la kuhakikiwa vitambulisho
vya Taifa na Taarifa za utumishi wa umma kwenye siku kuu ya idd
kitendo ambacho kinaonekana kuingilia uhuru wa kuabudu.
Haya yamesemwa wakati wa ibada ya baraza ambalo limefanyika kwenye
msikiti wa ijumaa uliopo Kata ya Kalangalala Wilaya na Mkoa wa Geita Siku
ya Jana .
Akizungumza juu ya hatua hiyo Mwenyekiti wa halmashauri
kuu ya BAKWATA Mkoani humo ,Alhaji Said Karidushi
,amesema kuwa nchi yetu inaheshimu uhuru wa kuabudu na kwamba swala
la wengine kwenda kuswali na wengine kuakikiwa vyeti ni jambo ambalo sio la
kiungwana na wala sio la kizarendo.
“Nimesikitishwa sana Mkuu wa Wilaya na Kitendo ambacho leo kimeendelea
nimeshahudia kwa macho yangu watumishi wakifanyiwa uhakiki siku ya
leo(jana)Jambo ambalo sio nzuri nchi yetu imeweka siku ya leo kuwa ya mapumziko
kuanzia ngazi mbali mbali za kiutumishi sasa nasikitika kuona wengine
wakiendelea na shughuli swala hili ni kuwanyima watu haki ya kuabudu”Alisema
Karidushi.
Aidha kwa upande wake Sheikh Mkuu wa Mkoa huo,Alhaji Yusufu
Kabaju,amesisitiza kuwa kitendo ambacho kimefanyika sio kitendo
chema na kwamba kwakua kimefika kwa mkuu wa Wilaya ni vyema wakafanyia
kazi ili yasije kujitokeza mambo ya namna hiyo kwa kipindi cha Mbeleni .
Akijibu baadhi ya matatizo ambayo yamewakilishwa mbele yake Mkuu wa
Wilaya ambaye ndiye alikuwa mgeni Rasmi kwenye shughuli ya baraza hilo amesema
kuwa mambo ambayo yanashida na ambayo wameyaeleza hataakikisha anayafanyia kazi
kwa kuandika barua ya maelekezo kwa wakuu wa idara mbali mbali .
Waumini wa Dini ya Kislamu wamemaliza Mfungo wa siku 30 wa mwezi
mtukufu wa ramadhani ambapo ni moja kati ya nguzo muhimu kwenye dini
hiyo.
No comments:
Post a Comment