Mwenyekiti wa kitongoji cha Mwabalogi Kijiji cha Kifufu ambaye ambaye ametengwa na wananchi kutokana na kugoma kulipa faini ya shilingi laki sita. |
Diwani wa kata ya Bugalama , Luponya Masalu akiwasisitiza wananchi kuishi kwa amani na kusameheana makosa yao ili kuruhusu maendeleo kwenye Kijiji cha Kifufu. |
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza Diwani wakati alipokuwa akihutubia hadhara hiyo. |
Wakina Mama wakifuatilia Mkutano huo. |
Meza kuu ikiongozwa na Mwenyekiti pamoja na wajumbe wa kikao hicho. |
Hata hivyo mwenyekiti huyo Bw Nchemba Kasomeko amesababisha hali ya
sintofahamu kwa wanakijiji baada ya kugoma kuomba msamaha na kukiri makosa
ambayo yamesababishwa na watoto wake mbele ya mkutano wa hadhara ulioitishwa na
diwani wa kata hiyo uliokuwa na lengo la kuleta suluhu baina yake na wanakijiji
kutokana na tuhuma za kuwahifadhi wahalifu wakiwemo wajukuu zake jambo ambalo
limesababisha uvunjifu wa sheria.
Katika Mkutano huo Bw Nchemba anadaiwa kuwakejeli wananchi pamoja na
viongozi wa kata wakiongozwa na Mwenyekiti wa kamati ya maendeleo ya kata hiyo
baada ya kumtaka alipe faini ya Sh Laki 6 ya kuhifadhi wahalifu baada ya
wajukuu zake kutuhumiwa kwa wizi wa matikiti maji kwenye shamba la Leonard
Martin kwa kuwaita masikini.
“Ndugu zanguni mimi nashangaa watu kusongamana kila wakati mnanitafuta
mimi tu,nimekuwa kama dume la wizi na nyie viongozi hapa mbele ni wanafiki tu
na kitu cha kukaa ninasumbuliwa nitoe laki sita wakati sio mwizi wizi ni
watoto mliwaachia nyie kuwa mmewasamehee leo tena mnataka nitoe mahela mengi
wanakijiji nilishawai kufika kwako nikakomba mboga tatizo umasikini wenu
unawasumbua au mnataka nitoke humu nijenge Geita”Alifoka kwenye Mkutano huo.
Kutokana na Majibu ya Nchemba kuwa ya kejeli na kuto kuafiki kulipa faini
ya Sh Laki 6, baadhi ya wananchi wamechukizwa na kauli zake na kuuomba uongozi
wa kijiji na kata kuondoka nae .
“Kweli Nchemba asijione anavyo
sana kuliko wananchi kama kuna faini naomba atoe hiyo faini sio yeye ajifanye
anavyo sana jamani kwani Mungu aliumba Masikini na matajiri” Alisema
Getruda Kachwele.
“Ndugu mwenyekiti nadhani Muda unakwenda na hili
la Nchemba hatutalimaliza sisi tulikwisha wapatia mtu wenu mnaonaje kama
mtamchukua muende nae tu maana sisi huyu hatuwezi kuendelea kuwa na mtu wa
namna hii kijijini hapa” Alisikika akisema
Musa Msafiri.
Kufuatia madai hayo kwa wananchi Diwani wa kata Hiyo, Luponya Masalu
amemtaka Bw Nchemba kuwaomba radhi wananchi na kuwalipa wananchi pesa ya faini
ambayo anadaiwa lakini amekaidi na kumtaka diwani kumuacha akajifikirie.
Julai 23 Mwaka huu Mkutano Mkuu wa Kijiji hicho uliketi na kuazimia Bw,
Nchemba alipe kiasi hicho cha fedha ambapo alikubali lakini leo ameyatupilia
mbali maamuzi hayo .
No comments:
Post a Comment