Thursday, 25 May 2017

MAHENGE AVAA KIATU CHA ALPHONCE MAWAZO GEITA

Mwenyekiti aliyechaguliwa wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA,Fabian Mahenge Akiomba kura kwa wajumbe wakati wa mkutano wa maamuzi ya uchaguzi wa ndani ya chama hicho.

Mgombea wa uenyekiti Bw,Charles Makanje akiomba kuchaguliwa wakati wa uchaguzi wa mwenyekiti ngazi ya Mkoa ndani ya chama cha CHADEMA.


Miongoni mwa wasimamizi wa uchaguzi huo,ambaye ni Afisa wa kanda wa chama Mayala Marthin Akionesha karatasi ya uchaguzi mbele ya wajumbe.

Uchaguzi ukiendelea moja kati ya wajumbe akidumbukiza kikaratasi kwenye chombo cha uchaguzi.

Uchaguzi ukiendelea moja kati ya wajumbe akidumbukiza kikaratasi kwenye chombo cha uchaguzi.

Wajumbe wakifuatilia uchaguzi huo.

Msimamizi wa uchaguzi ambaye ni Katibu wa kanda ya ziwa wa  chama hicho,Bi Rehema James Mkoha akitangaza matokeo ya uchaguzi huo.
Msimamizi wa uchaguzi ambaye ni Katibu wa kanda ya ziwa wa  chama hicho,Bi Rehema James Mkoha,akimkabidhi  hati ya ushindi  Fabian Mahenge ambaye ndio mwenyekiti wa chama hicho ngazi ya Mkoa.



Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Geita ,Fabian Mahenge akiwashukuru wajumbe kwa kumpigia kura na kumpa nafasi ya kuwaongoza ndani ya chama hicho.



Chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema) Mkoani Geita kimefanya uchaguzi wa ngazi ya mwenyekiti kwaajili ya kuziba nafasi ya  aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho,Mkoani humo Alphonce Mawazo aliyeuwawa  mwezi wa kumi na moja  mwaka 2015 huko kwenye Kijiji cha Ludete Halmashauri ya mji mdogo wa katoro.

Uchaguzi huo ulianza majira ya saa Sita na kumalizika saa kumi na moja jioni na msimamizi akiwa ni Katibu wa kanda ya ziwa wa  chama hicho,Bi Rehema James Mkoha ambaye aliwatangaza wagombea wa kiti hicho kuwa ni Fabian Mahenge na Charles Makanje.

Hata hivyo pamoja na kuwepo kwa figisu figisu kwa baadhi ya wajumbe kuonekana kutoa rushwa Msimamizi wa uchaguzi aliwaonya wenye tabia za namna hiyo kuachana nazo mala moja kwani uchaguzi huo unazingatia misingi ya haki kama ilivyo ndani ya katiba ya chama hicho.

Bi,Mkoha akiwa kama msimamizi wa uchaguzi huo alimtangaza Fabian Mahenge kuwa ni msindi wa kiti hicho kwa kura 35 sawa ni asilimia 61.4 huku mgombea Mwingine Bw,Charles Makanje akipata kura 22 sawa na asilimia 61.4.

Hivyo kutokana na matokeo hayo Msimamizi wa uchaguzi huo alimtangaza Bw ,Fabian Mahenge kuwa  mrisi wa nafasi ya aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho ngazi ya Mkoa Alphonce Mawazo aliyeuwawa tarehe 14 mwezi wa 11 mwaka 2015 na kuzikwa tarehe 30 mwezi wa 11 mwaka 2015.

Kwa upande wake mwenyekiti ambaye amechaguliwa Bw,Fabiani Mahenge  amewahidi wanachama  kuwatumikia  kwa kujitoa pamoja na kuwa na mshikamono huku akikemea swala la matabaka ndani ya chama na kuwataka wanachama kuwa wamoja katika kutetea masirahi ya chama hicho.

Uchaguzi huo ulikuwa na  idadi ya ya wapiga kura waliojisajiri 59 ,idadi ya kura ambazo zimepigwa ni 57 halali 57 na ambao hawakupiga kabisa ni 2.



No comments:

Post a Comment