Mkuu wa mkoa wa Geita Meja
Jenerali Mstaafu Ezekiel Elias Kyunga
amesema kuwa miradi mbalimbali
inayoanzishwa na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM), bado haieleweki kwa Wananchi hali
ambayo inasababisha kuwepo kwa malalamiko mengi.
Kyunga ametoa kauli hiyo
wakati akizungumza na waandishi
wa habari baada ya kumalizika kwa kikao cha kujadili namna ambavyo halmashauri
ya wilaya na mji geita watakavyoweza kuwashirikisha Wananchi katika miradi inayoanzishwa na Mgodi
huo.
Amesema kuwa imefikia hatua Wananchi wanautuhumu mgodi huo kuwa hauna
manufaa yoyote kwao jambo ambalo limewalazimu kuketi kujadili baadhi
ya mambo yatakayoeleweka kwa
jamii.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita Marx Kamaoni
amesema kuwa miongoni mwa matumizi
yaliyofanyika kutokana na fedha za ushuru
wa huduma kwa jamii
zilizotolewa na Mgodi (service levy)
zimenunulia mitambo ya kutengenezea barabara iliyogharimu kiasi cha Sh.Bilioni 1.2.
Hata hivyo kumekuwepo na malalamiko kutoka kwa baadhi ya madiwani wa
halmashauri zote mbili kupinga
utaratibu uliowekwa na halmashauri
hizo kuwa atakayetaka kurekebisha
miundombinu katika eneo analotoka
aweke mafuta kwa gharama zake.
No comments:
Post a Comment