Akizungumza katika
hafla ya kuwaaga wagonjwa wenye tatizo la midomo sungura Kaimu mkurugenzi wa
mgodi wa dhahabu wa Geita, Habati Cawoodi amesema kuwa mgodi huo umefurahishwa na zoezi hilo,
ambalo walilianza mwaka 2004 na kwamba
jumla ya watu elfu 1,200 wamekwisha kufanyiwa upasuaji na wakarudi
katika hali yao ya kawaida.
Akimwakilisha mkuu wa
wilaya, Kaimu katibu mkuu wa wilaya ya Geita Saashisha Magwe,ameeleza kuwa ni
vyema kwa wananchi wenye matatizo ya midomo sungura kujitokeza na kutokuendelea
kukaa na ugonjwa huo kwani unatibika.
Meneja wa mawasiliano
na mahusiano mgodi wa GGM, tenga bintenga, amesema furaha ya mgodi ni kuona namna watu
wanaporejea wanakuwa wako katika hali
nzuri na yenye furaha.
Aidha kwa upande wao
wananchi na wazazi wa watoto wenye matatizo hayo wameushukuru mgodi wa ggm
namna ambavyo umeendelea kuwajali
wananchi na kutoa huduma za afya ambazo ni za bure.
No comments:
Post a Comment