Friday, 1 June 2018

WANANCHI WASHIRIKIANA NA SERIKALI KUJENGA ZAHANATI MKOANI GEITA







Wananchi wa kijiji cha Bwiyegure Kata ya mtakuja Wilaya na Mkoa wa Geita wameamua kuanzisha ujenzi wa Zahanati kwa kushirikiana na serikali lengo likiwa ni kukabiliana na tatizo la kutembelea umbali mrefu kufuata huduma za afya hali ambayo imekuwa ikisababisha baadhi yao kupoteza maisha kutokana na kukosekana kwa huduma hiyo.


Hatua hiyo imetokena na hivi karibuni wanawake wa Kijiji hicho kuchimbishwa kaburi kwa imani kuwa wamekuwa wakishiriki vifo vya wanaume ambavyo vimekuwa vikijitokeza mara kwa mara kijijini hapo.

Wakizungumza na  Storm habari Kijiji hapo baadhi ya wananchi wamesema kuwa wamekuwa wakipata shida kubwa ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya  hali ambayo inapelekea wengine kujikuta wakiwapeleka wagonjwa kwa waganga wa kienyeji.

Diwani wa kata hiyo, Constatine Molandi amesema matarajio ni kuwa na zahanati kwa kila mtaa kwenye kata hiyo huku mtendaji wa kata,Bi Neema Yona akielezea matatizo ya wananchi kutokuwapeleka wagonjwa kwenye  zahanati kutokana na umbali wa huduma hizo.


Aidha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji,Mhandisi Modest Aporinaly ameelezea Bajeti ambayo wamepanga kwa mwaka huu kwa ujenzi wa zahanati na vituo vya afya,huku Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akisisitiza wananchi kuendelea kushirikiana kwenye shughuli ya ujenzi wa zahanati hiyo.

No comments:

Post a Comment