Mratibu wa huduma za kifua kikuu na ukoma Halmashauri ya Wilaya Kizingi Madeni akitoa takwimbu ya ugonjwa wa TB.
Ikiwa leo ni siku ya kifua kikuu duniani imebainika kuwa
wagonjwa 522 Wilayani Geita wamegundulika kuwa na vimelea vya kifua kikuu
Akizungumza
na waandishi wa habari ,Mratibu wa huduma za kifua kikuu na ukoma Kizingi
Madeni,alisema tatizo la kifua kikuu ni
kubwa sana katika halmashauri ya wilaya hiyo.
“Tatizo la
Kifua kikuu kwa wilaya yetu ni kubwa ambapo ukiangalia takwimu za mwaka jana watu 522 wamegundulika kuwa na maambukizi ya
kifua kikuu na tangu January hadi February watu
105 wameathirika na tatizo hili ukiangalia takwimu hii unaona idadi ni kubwa
sana kwa hiyo bado inaitajika nguvu kubwa ikiwa ya kutoa elimu ya kifua kikuu”alisema
Madeni.
Miongoni mwa
maeneo ambayo yanaongoza kwa maambukizi ni pamoja na kwenye migodi ya uchimbaji
madini maduka online ilizungumza na Mganga Mkuu wa Mgodi wa dhahabu wa Geita(GGM)
Kiva Mvungi ambapo wao kama mgodi
wamekuwa wakishiriki kutokomeza kifua kikuu kwa kuchangia kwenye hospitali ya
Rufaa ya Mkoa kwa kutoa vifaa vya matibabu na kukarabati hodi za wagonjwa ikiwa
ni pamoja na kutoa elimu kwa wananchi na wafanyakazi.
“Kwasababu
ya watu wanaotuzungukuka kuakikisha kwamba wanajikinga na kifua na wanatibiwa
pasipo matatizo tumekarabati hospitali ya Mkoa ikiwa ni pamoja na kutoa vifaa
vya matibabu lakini pa tumeendelea kutoa elimu kwa kushirikiana na halmashauri
zote mbili”alisema Mvungi
Elibariki
Mussa ni moja kati ya wananchi Mkoani
Geita ameshauli elimu kuendelea kutolewa zaidi kwani bado tatizo lililopo ni wananchi
wengi hususani ni maeneo ya machimbo awana elimu juu ya maambukizi ya kifua
kikuu.
Siku ya kifua kikuu duniani huadhimishwa Tarehe 24 Mwezi March kila
mwaka ambapo kwa mwaka huu Kauli mbiu ni“Tuungane kutokomeza kifua kikuu”
|
No comments:
Post a Comment