Bunge limekanusha
taarifa inayosambazwa katika mitandao ya kijamii na watu wanaodaiwa kuwa ni
madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.
Taarifa hiyo inadai
kuwa video iliyomuonesha aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles
Kitwanga akijibu swali bungeni Mei 20 mwaka huu, ilihaririwa na kusambazwa na
maafisa wa Bunge.
Kitengo cha Habari,
Elimu na Mawasiliano cha Bunge kilitoa taarifa ya ufafanuzi kuhusu madai ya
kuhaririwa kwa video hiyo, mjini Dodomajana.
Taarifa hiyo ilieleza
kuwa taarifa hizo, si za kweli na zina lengo la kuupotosha umma, kwani ukweli
ni kwamba kipindi cha maswali na majibu bungeni, hurushwa moja kwa moja na
hupatikana kupitia vituo vyote vya televisheni, vinavyopokea matangazo ya
bunge.
Ilisema matangazo
hayo, yanaweza pia kurekodiwa na mtu yeyote mwenye uwezo huo popote alipo,
kadri anavyoweza kuyapokea matangazo.
No comments:
Post a Comment