Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita,Ali Kidwaka akisisitiza waandishi kuwa
na umoja na mshikamano katika kutetea na kulinda haki zao za msingi kwenye
shughuli ambazo wanazifanya Hayo ameyasema leo kwenye siku kuu ya uhuru
wa Vyombo vya habari ambayo yamefanyika kwenye ukumbi wa Seft Park Mjini Geita.
Mkuu wa
Wilaya ya Geita Mwl,Herman Kapufi akizungumza na waandishi wa Habari juu ya
umuhimu wa Siku hiyo.
Waandishi wa
habari na viongozi mbali mbali wakiwa kwenye Picha ya pamoja wakati wa
maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya Habari.
Waandishi wa habari Wilayani na Mkoani Geita wametakiwa
kuandika habari zenye ubora na zenye kuleta chachu ya maendeleo katika jamii.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Mtendeji wa halmashauri ya Wilaya
ya hiyo Bw Ali Kidwaka wakati wa sherehe za Maadhimisho ya siku ya Uhuru
wa Vyombo vya habari yaliyofanyika ki Mkoa mjini Geita .
Amesema ili kuleta maendeleo katika Taifa na jamii kwa ujumla waandishi
wa habari wanapaswa kuandika habari zenye ubora na zisizokuwa na upendeleo
ambazo zitasaidia kwa kiasi kikubwa watu kujitambua katika kuleta maendeleo ya
Taifa na Jamii kwa ujumla.
Pia amewataka kuendeleza ushirikiano na taasisi mbalimbali ili
kuweza kuibua changamoto ambazo zitaleta maendeleo.
Kwa upande wake Mgeni rasmi katika sherehe hizo ambaye pia ni mkuu wa
Wilaya hiyo,Mwl Herman Kapufi amesema kuwa ni vyema kwa waandishi kutumia muda
mwingi wa kujifunza maeneo ambayo kwao bado yanautata pia kuwa wazalendo na
kushikamana kwa pamoja
Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Geita Daniel Limbe
amempongeza mkuu wa Wilaya ya Geita Pamoja na wadau wengine kuwa bega kwa bega
katika kuwasaidia waandishi ambao wapo wilayani Geita.
“kauli mbiu ya maadhmisho hayo ni klabu za waandishi wa
habari zina wajibu wa kuendeleza amani katika jamii” ambapo Kitaifa
yameadhimishiwa Jijini Mwanza.
No comments:
Post a Comment