Miss Tanzania 2016, Diana Edward
Waziri wa Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye amesema serikali
haijamtelekeza mshindi wa shindano la Urembo la Tanzania kwa mwaka 2016 bali
wanaendelea kumpa msaada wa hali na mali ili kufanikisha ushiriki wake katika
mashindano ya urembo ya dunia.
Mhe. Nape ameyasema
hayo jana Jijini Dar es Salaam alipokuwa akikabidhi Bendera ya Taifa kwa
mshiriki kutoka Tanzania anayekwenda kushiriki mashindano ya Miss Afrika 2016
yatakayofanyika Novemba 28 mwaka huu.
“Haiwezekani Serikali
ikabariki mchakato mzima wa Miss Tanzania mshindi akapatikana alafu
akatelekezwa na tukakaa kimya sio kweli” Alisistiza Mhe. Nnauye.
Mhe. Nnauye ameongeza
kuwa watanzania wawe na desturi ya kutangaza mambo mema yanayotokana na
shindano hilo la urembo badala ya kutafuta mapungufu na kuyakuza na yakaonekana
kuwa ni tatizo kubwa katika machakato huo.
Aidha amewahakikishia
watanzania kuwa Miss Tanzania yuko salama na atashiriki vizuri katika
mashindano ya Miss World kwa mwaka 2016 watanzania wazidi kumwombea na
ikiwezekana kwa mwaka huu mrembo wa Dunia atokee Tanzania.
Katika mashindano ya
urembo kwa mwaka 2016 mrembo yaliyofanyika Jijini Mwanza na Bi Diana Edward
Luqumay alishinda taji hilo na anatarajia kuiwakilisha Tanzania katika
mashindano ya Urembo ya Dunia 2016 yatakayofanyika mwishoni mwa mwaka huu
Washington Dc nchini marekani na yatashirikisha nchi 119.
No comments:
Post a Comment