Bodi ya Mikopo ya
Wanafunzi wa Elimu ya Juu inapenda kukanusha taarifa zinazosambazwa kupitia
mitandao mbalimbali ya kijamii kuwa imetangaza sifa na vigezo vitakavyotumika
katika uchambuzi wa maombi ya mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo
2016/2017.
Taarifa hizo
zinazosambazwa, pamoja na mambo mengine, zinaeleza kuwa sifa zitakazotumika
kuwa ni ufaulu wa waombaji katika mitihani yao ya elimu ya sekondari na
diploma. Aidha, taarifa hizo zinaeleza kuwa maelezo rasmi yanapatikana katika
tovuti ya Bodi ya Mikopo na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU).
Bodi inapenda
kuwataarifu wadau wake wote, wakiwemo wale wanaotarajia kuomba mikopo ya elimu
ya juu kuwa taarifa hizo sio za kweli na kuwaomba wawe na subira wakati Bodi
inakamilisha taratibu za uombaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2016/2017.
Baada ya kukamilika
kwa taratibu hizo, mwongozo wa utoaji mikopo utatolewa rasmi na kutangazwa kwa
umma kupitia njia mbalimbali vikiwemo vyombo vya habari na tovuti ya Bodi ya
Mikopowww.heslb.go.tz
IMETOLEWA NA:
KAIMU MKURUGENZI
MTENDAJI,
BODI YA MIKOPO YA
WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU,
JUMANNE, JUNI 7, 2016
Taarifa hii pia
inapatikana katika tovuti ya Bodi (www.heslb.go.tz)
No comments:
Post a Comment