Wananchi wa mtaa wa Mwembeni kata ya Nyankumbuku mkoani Geita wameendelea kusisitiza kuwa
hawataondoka katika maeneo ambayo yanasemekana
kuwa ni ya jumuiya ya wazazi wa chama cha mapinduzi kutokana na kwamba
maeneo hayo wana uhalali wa kuyamiliki.
Wakizungumza mbele ya diwani wa kata ya Nyankumbu katika mkutano wa kujadili hatma ya maeneo ambayo waliambiwa na
mkuu wa wilaya ya Geita, Mh Manzie Manguchie kuyaachia na kuacha kufanya
shughuli yoyote.
Wamesema kuwa jumuhiya ya wazazi,waliwaruhusu mbele ya
mahakama kuwa waendelee na shughuli zao sababu
ya kukosekana fedha za
kuwafidishia,swala ambalo liliwapa wasi wasi ni baada ya mkuu wa wilaya
kuwataka kuondoka maeneo hayo kwa madai kuwa si maeneo yao ni ya jumuhiya hiyo.
Diwani wa kata ya nyankumbu michael kapaya amesema kuwa swala hilo lipo
kinyume na makubaliana kutokana na kwamba vielelezo vipo na vinaonesha kuwa
jumhiya hiyo ilishindwa gharama na kwamba hawatakubaliana na hatua ambayo
inataka kuchukuliwa kwa kuwaondoa wananchi maeneo yao.
Aidha,mkuu wa wilaya ya Geita Manguchie
amesema kuwa tatizo lililopo katika eneo hilo ni uwelewa na kwamba wanatakiwa
kujua kuwa kabla ya kutaka kujenga ni vyema wakapata kibali cha ujenzi na
kwamba juu ya eneo hilo kuna hati ya ardhi ambayo inawatambua wamiliki ni
jumuhiya ya wazazi.
No comments:
Post a Comment