Wananchi wa mji mdogo
wa Katoro wilayani Geita, wameendelea kuishukuru kampuni ya uchimbaji wa madini
ya dhahabu (GGM),kwa kutoa msaada wa matibabu kwa waathirika wa midomo sungura.
Storm habari
imezungumza na baadhi ya wazazi ambao walikuwa na watoto wenye tatizo
hilo,ambapo wamesema kuwa kabla ya kupatiwa msaada wa upasuaji wa watoto wao
hali ilikuwa ni tofauti kutokana na kukosa gharama za matibabu.
Mganga mfawidhi wa
kituo cha afya Katoro, Peter Janga
amesema tatizo hilo ni kubwa katika mkoa
wa Geita, na hali hiyo inaonekana kukithiri kutokana na kwamba kila mwezi huwa wanapokea takribani watoto
watatu.
Theophil Pima ambae ni
Afisa Mawasiliano mwandamizi wa mgodi huo,amesema toka mwaka 2001 hadi hivi
sasa kampuni ya GGM imegharamia matibabu takribani wagonjwa 700,na zoezi hili ni endelevu kutokana na
kaulimbiu yao ya jamii inayozunguka mgodi lazima ifaidike na uwepo wa mgodi
huo.
Akizungumza kwa niaba
ya Serikali Afisa habari halmashauri ya wilaya ya Geita Bi.Trovina Kikoti
amesema kuwa serikali inatoa shukrani za dhati kwa GGM,kwa kutoa msaada wao kwa
ajili ya matibabu pia ameishauri jamii isiwafiche watoto ndani wenye matatizo hayo kwani yanatibika
No comments:
Post a Comment