Ubovu wa miundombinu ya
Barabara na ukosefu wa huduma za afya
katika kijiji cha Lubando kilichopo kata ya Shabaka wilayani Nyang`wale
mkoani hapa,ni sababu ya akina mama wengi hususani wajawazito kujifungulia
njiani na wagonjwa kupoteza maisha
kutokana na kufata zahanati katika kata ya kasamwa.
Wakizungumza na storm
habari,wananchi wa kijiji hicho wamesema kuwa wamekuwa wakitembea umbali wa
kilomita 17 na kutokana na ubovu wa barabara ya kuelekea Kasamwa ambapo ndio
panapatikana huduma hiyo imekuwa ikipelekea wagonjwa wengi kupoteza maisha na
wakina mama kujifungulia njiani.
Bw. John Magagala ni
mkazi wa kijiji hicho ameeleza kuwa suala la ubovu wa barabara ni sababu ambayo
imekuwa ikipelekea kukosekana kwa
usafiri katika kijiji hali ambayo imekuwa ikisababisha wagonjwa wengi kupoteza
maisha pindi wanapokuwa njiani kuelekea kutafuta huduma ya kituo cha afya hii
ni kutokana na kutokuwapo kwa kituo cha afya kijijini hapo.
Kwa upande mwingine
Bi.Naomi Lunemya ni miongoni mwa
wahanga amesema kuwa kutokana na kukosekana
kwa huduma za afya katika ngazi za vijiji akina mama wengi wamekuwa
wakihangaika kutokana na kukosekana kwa huduma ya afya.
Odelo Rastilajula amesema kuwa wanawake wengi
wamekuwa wakipata shida kupata huduma ya afya kutokana na umbali wa kilomita 17
kutoka lubando hadi kasamwa hali ambayo
imekuwa inasababisha akina mamawengi kujifungulia njiani.
Hata hivyo storm habari
ilipomtafuta diwani wa kata ya shabaka kwa njia ya simu kujua anajitihada gani za kuhakikisha
anaboresha kata yake ikiwa ni pamoja na miundombinu ambayo wananchi wake
wamemlalamikia hakuweza kupatikana.
No comments:
Post a Comment