Monday, 25 April 2016

WAFANYABIASHARA MKOANI GEITA WALALAMIKIA KUTOZWA USHURU WA JUU

Wafanyabiashara katika soko  linalomilikiwa na chama cha mapinduzi (ccm) kata ya Katoro wilayani na mkoani  Geita wamelalamikia kuwepo kwa gharama kubwa ya utozwaji wa ushuru.

Wakizungumza  na  Storm habari  kwa nyakati tofauti baadhi ya wafanyabiashara katika soko hilo wameeleza kuwa kumekuwepo na ushuru ambao hauna utaratibu mzuri kwani huwalazimu kulipa mara 2 kwa siku,  jambo ambacho linawatatiza sana kulingana na uchumi wao kuwa  duni.

Kwa  upande wake mwenyekiti wa tawi la ccm katika kata hiyo bw, Mlukwa Ndigayi  amesema kuwa ushuru unaotozwa katika soko hilo ni kwa ajili ya usafi  wa eneo hilo la biashara na siyo kwamba wanaibiwa kwani  ni kitu ambacho walijipangia wao pamoja na viongozi wa chama cha mapinduzi (ccm)  ambao ndiyo wamiliki wa soko hilo.

No comments:

Post a Comment