Saturday, 2 April 2016

VIONGOZI NA WANANCHI WA MTAA WA KATORO MKOANI GEITA WADHIBITI SUALA LA AJALI ZA BARABARANI.


Viongozi wa Serikali ya mtaa wa Katoro wakishirikiana na wananchi wameshiriki zoezi  la uwekaji matuta katika baadhi ya barabara  za mitaa kutokana na kuwepo kwa ajali nyingi zinazohusisha watoto wa shule kugongwa na magari.

wakizungumza na storm habari baadhi ya wakazi walioshiriki zoezi hilo  wamesema kuwa  sababu kubwa iliyopelekaea kuweka matuta hayo ni kutokana na kuwepo kwa ajali ambazo  zinahusisha watoto wadogo wa shule  kugongwa na vyombo mbalimbali vya moto.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kata hiyo Bw.Japheti Madoshi amesema kuwa  baada ya kutengenezwa kwa barabara kubwa ya mtaa kumeonekana  kuwa  na mwendo kasi kwa vyombo vya moto  hali ambayo imepelekea  kuashiria hatari kwa watembea kwa miguu

No comments:

Post a Comment