Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit akipokea maua kutoka kwa
mtoto Sharon Innocencia Shiyo mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Ikulu
jijini Dar es Salaam na kulakiwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano
Dkt. John Pombe Magufuli.
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit akisalimiana na Makamu wa
Rais Samia Suluhu Hassan mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu jijini
Dar es Salaam kwa ajili ya Utiaji saini wa Mkataba wa kujiunga na Jumuiya ya
Afrika Mashariki.
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit akisalimiana na Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu kwa ajili ya
Utiaji saini wa Mkataba wa kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit akikagua Gwaride la Heshima
mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit akiwa amesimama na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wimbo wa Taifa ukipigwa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. John Pombe Magufuli akitia saini kwenye
mkataba wa kuiwezesha Jamhuri ya Sudan Kusini kuwa Mwanachama
kamili wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. John Pombe Magufuli akibadilishana makabrasha
ya mkataba na Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit mara baada ya kukamilika
kwa zoezi la utiaji Saini wa kuiwezesha Jamhuri ya Sudan Kusini kuwa Mwanachama
kamili wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Rais wa
Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit kabla ya utiaji saini wa Mkataba wa Sudani
Kusini kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. Magufuli akitoa hotuba yake mara baada ya zoezi la utiaji
Saini kukamilika.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais
wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit wakipiga makofi mara baada ya kufurahishwa
na wimbo wa bendi ya Polisi iliyokuwa ikitumbuiza Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya
ya Afrika Mashariki Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja
na mgeni wake Rais wa Sudan Kusini Salva
Kiir Mayardit pamoja na viongozi wengine, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan
watatu kutoka kushoto na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa watatu kutoka kulia.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia wakati Bendi ya Matarumbeita
ilipokuwa ikitumbuza Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na IKULU
No comments:
Post a Comment