Serikali wilayani Chato mkoani Geita imejipanga
kuhakikisha kuwa inaimarisha swala la ulinzi na usalama kwa kuwatumia
wajumbe wa nyumba kumi.
Hayo yamesemwa na mkuu
wa wilaya hiyo, Shabaani Ntarambe wakati
akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.
Amesema kuwa katika kuhakikisha
kuwa ulinzi na usalama unaimarishwa watahakikisha kuwa wanawatumia wajumbe
wa nyumba 10 kwa kuhakikisha kuwa wanaangalia wale wote ambao wanaingia
katika kaya wanazoziongoza.
Mh.Ntarambe ameongeza
kwa kuwataka wananchi kuhakikisha kuwa wanafanyia kazi swala la uhakiki wa silaha
zoezi ambalo limeanza jana Aprili 1 na linatarajia kumalizika june 30 mwaka
huu.
Aidha amewataka wananchi
katika zoezi hilo la kuhakiki silaha kuwa na maelewano kwa wananchi kuwa na
hiyari ya kusalimisha silaha zao.
No comments:
Post a Comment