Mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa kazi ya kutafuta watumishi hewa katika
manispaa za jiji la Dar es Salaam bado linaendelea baada kubaini njia chafu
wanazotumia watumishi hewa hao.
Akizungumza leo na
waandishi habari ,Makonda amesema kuwa Mkoa wa Dar es Salaam ni kioo kwa nchi
hivyo jitihada zinaendelea ya kutafuta na kazi hiyo itafanywa sekta kwa sekta.
Amesema kuwa Wakuu wa
Wilaya katika jiji la Dar es Salaam hakuna kufanya kazi yeyote mpaka wamelize
kutafuta watumishi hewa kwa kutumia malipo ya watumishi kutoka taasisi za
fedha (Pay low).
Makonda amesema idadi
ya watumishi hewa 71 aliowasilisha kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais –Tamisemi,
Georgre Simbachawene ni ndogo katika jiji la Dar es Salaam hivyo
kazi lazima iwe endelevu.
Amesema kuwa watumishi
Hewa hawawezi wakawa wanalipwa mshahara huku wanaofanya kazi kwa moyo mmoja
wanajisikia vibaya hivyo ni lazima watafutwe na wachukuliwe hatua na
vyombo vya dola.
Mkuu Mkoa amesema kuwa
kati ya watumishi hewa 71 ni watumishi 34 hewa wamefunguliwa mashitaka katika
mahakama mbalimbali kutokana kuchukua fedha wasioifanyia kazi.
No comments:
Post a Comment