Watu kumi na moja wameripotiwa kuwa na ugonjwa wa Kipindupindu katika mji mdogo wa Katoro mkoani Geita ambao unasadikika kuibuka kwa mara nyingine kuanzia jana machi 31baada ya watu wanne kugundulika kuwa na dalili za ugonjwa huo.
Akizungumza na Storm habari mganga mfawidhi wa kituo cha afya Katoro bw Peter Janga , amesema kuwa amepokea watu kumi na moja wanaodaiwa kuwa na ugonjwa wa kipindupindu na kwamba kwa sasa wanaendelea kufanyiwa matibabu katika kituo hicho.
Kwa upande wake mwenyekiti wa mamlaka ya mji mdogo wa Katoro bw Japheti Madoshi amekiri kuwepo kwa wagonjwa wa kipindupindu katika kituo hicho na kwamba
wameweka mikakati madhubuti ya kukabiliana na ugonjwa huo ambao umekuwa hatarishi
katika maisha ya wananchi nchini.
Aidha mwenyekiti huyo amewataka wananchi wa mji huo
kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na kusafisha mazingiza
yao kuchemsha maji ya kunya na kuacha kutumia vyakula vya baridi hali ambayo
itawasaidia kujikinga na maabukizi ya ugonjwa huo.
No comments:
Post a Comment