Wednesday, 20 April 2016

WANANCHI MKOANI GEITA WALALAMIKIA KUPANDA KWA BEI SUKARI

Wananchi  mkoani Geita wamelalamikia suala la wafanyabiashara wa sukari kupandisha gharama kutoka katika bei ya shilingi 2000 hadi kufikia shilingi 2500 hali ambayo imekuwa ni changamoto kubwa hasa kwa wananchi wenye vipato vya chini
Wakizungumza na Storm habari   wananchi hao wamesema kuwa suala hilo limekuwa likiwapa changamoto kubwa kwani  kutokana na kushindwa    kununua sukari  ambayo imekuwa ikipanda siku hadi siku .
Aidha  wafanyabiashara mkoani  hapa wamesema kuwa suala hilo  limesababishwa na upatikanaji wa bidhaa  kuwa ghali huku wengine wakidai kuwa ni kutokana na kuzuiliwa  uingiaji  kwa sukari  iliyokuwa ikitokea  nje ya nchi.

Kutokana na hali ya sukari kuwa juu wafanyabiashara wameiomba serikali kuruhusu sukari ya nje kuingizwa nchini jambo ambalo litasaidia kupunguza  adha  na uhaba wa sukari.

Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh Dkt John Pombe Magufuli february 18 alipokutana na makundi     mbalimbali yaliyoshiriki katika kampeni za uchaguzi mkuu 2015
wakiwemo wasanii alipiga marufuku   uagizaji wa sukari kutoka nje ya nchi ili kulinda na kuviendeleza viwanda vya hapa nchini.

No comments:

Post a Comment