Madereva wa
vyombo vya moto mkoani Geita wameshauriwa kuhakikisha wanafuata kanuni na sheria za barabarani ili kuepusha ajali ambazo zimekuwa
zikitokea mara kwa mara na kusababisha vifo
vya watanzania wengi.
Hayo
yamesemwa na mwakilishi wa mkuu
wa kitengo cha usalama barabarani (RTO) mkoani hapa,sajenti Deus Mgema,wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya usalama barabarani yanayotolewa na taasisi isiyo ya kiserikali
ya Greenmood Organization.
Amesema kuwa
ni vyema kwa dereva anapokuwa
barabarani kuwa na nidhamu pindi anapokuwa akiendesha chombo cha moto ikiwa ni pamoja
na kufata kanuni za usalama.
Kwa upande wake,bw Falesi Lujoja,amesema kuwa ni
vyema kwa wanafunzi ambao wamekuwa wakijitokeza kwenye mafunzo hayo
kutilia maanani kile wanachofundishwa.
Aidha mkurugenzi wa taasisi hiyo,Daniel Makungu,ameeleza dhumuni la kufungua taasisi
hiyo ni kuhakikisha kila mtu anayetumia barabara anarudi akiwa salama nyumbani na
kudhibiti ajali za mara kwa mara.
No comments:
Post a Comment