Rais Magufuli ametoa mchango wa shilingi milioni 10 kwa kanisa
la bikira Maria Parokia ya Chato Mkoani Geita kwa ajili kuchagia upanuzi wa
kanisa hilo ambapo fedha hizo zimekabidhiwa na kaimu mnikulu Ngusa Samike
katika misa ya pili ya ibada ya Jumapili ya pili ya Pasaka, iliyofanyika
kanisani hapo leo tarehe 03 April, 2016.
Kabla ya misa hiyo ya pili Rais Magufuli na mkewe Mama Janeth
Magufuli wakiwa pamoja na Waziri mkuu mstaafu wa Kenya Raila Odinga na Mkewe
Mama Ida Odinga, walisali misa ya kwanza ambapo Rais Magufuli aliahidi
kuchangia shilingi milioni 10 kwa ajili ya upanuzi wa kanisa hilo ambao
unaendelea.
Taarifa iliyotolewa na Ikulu imesema katika misa hiyo Paroko wa
Parokia ya Chato, Padre Henry Mulinganisa alieleza kuwa kanisa hilo linatarajia
kuadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwake baadaye mwaka huu, na kwamba
maadhimisho hayo yanakwenda sambamba na upanuzi wa kanisa ambao unachangiwa na
waumini wenyewe.
Padre Mulinganisa amemshukuru Rais Magufuli kwa mchango huo na
amemuahidi kuwa utatumika vizuri ili uendeleze upanuzi wa kanisa hilo pamoja na
michango ya waumini wengine.
No comments:
Post a Comment