Saturday 30 April 2016

MHANDISI MATHIAS SHOTO ASIMAMISHWA KAZI GEITA


Baraza la madiwani wa halamshauri ya wilaya ya Geita limemsimamisha kazi mhandisi wa halmashauri hiyo  Mathiasi Shoto,kwa  tuhuma za kushindwa kutekeleza majukumu yake ya kazi ikiwa ni pamoja na kushindwa kutaja barabara ambazo amekwishakamilisha tangu alipokabidhiwa uongozi huo.
Akitoa taarifa mbele ya baraza la madiwani, mwenyekiti wa halmashauri hiyo  Elisha Lupuga, amesema kuwa kamati ya madiwani imekaa na wajumbe na kuweza kubaini tuhuma ambazo zimepelekea mtumishi huyo kumsimamisha kazi.

Kwa upande wao madiwani wa halmashauri hiyo wamesema kuwa kusimamishwa kazi kwa mhandisi huyo kutatoa changamoto kwa watendaji wengine kufanya kazi kwa bidii ili kuleta maendeleo katika jamii.

Hata hivyo kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Geita,mh Manzie Manguchie ambaye alikuwepo katika kikao hicho amewataka watumishi wa serikali kuwa waamianifu na waadilifu huku akiwataka pia kuacha udanganyifu katika shughuli zao.


No comments:

Post a Comment