Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (takukuru) mkoani Geita inamshikilia bw,Shukurani Kulwa
Musa,kwa kufanya kazi ya uuguzi bila ya kuwa na sifa ambazo zinamruhusu kufanya
kazi hiyo.
Akizungumza na Storm
habari mkuu wa takukuru mkoani hapa,Thobias Ndaro, amesema kuwa taarifa za kupatikana kwa daktari huyo walizipata wiki moja kabla ya ujio wa waziri
mkuu na baada ya kufanya uchunguzi wa kina ulioweza kubaini kuwa bw,Shukurani hakuwa na sifa za kuwa daktari hali ambayo ilipelekea kumkamata kwa ajili ya
uchunguzi zaidi.
Ndaro
ameeleza kuwa kwa mjibu wa
uchunguzi ambao wameufanya walibaini
kuwa daktari huyo ni wale watu ambao wanafanya mazoezi ya vitendo na kwamba kwa
sasa bado wanaendelea na uchunguzi zaidi na utakapo kamilika watatoa taarifa
kamili juu ya daktari huyo.
AidhaStorm habari ilifanikiwa kufika katika ofisi za
mkurugenzi na kukutana na kaimu
mkurugenzi wa halamshauri ya wilaya,mwalimu Deus Self,ambapo amesema kuwa ni
kweli alipatiwa taarifa za mganga huyo ambae ni feki lakini
kwa madai ambayo mganga huyo alikuwa nayo alidai kuwa anajitolea katika
hosptali hiyo.
No comments:
Post a Comment