Mamlaka ya Usimamizi na udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA)imetangaza kushusha bei za umeme kuanzia
leo kwa watumiaji wote wa viwango tofauti.
Kushuka huko kwa bei
ya umeme ni kutokana na ombi la Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)kutaka bei
za umeme zipunguzwe sambamba na hilo gharama za huduma kwa baadhi ya wateja
zimeondolewa.
Bei mpya kwa
watumiaji wadogo ni sh.100 kwa uniti, watumiaji wa kati ni sh.292
toka 298 ya zamani.Wafanyabiashara wadogo ni sh. 195 toka sh.
200 ya hapo awali.
Bei mpya kwa wafanyabiashara wa kati ni sh.157 toka sh. 159. Wanaonunua kwa wingi (bulk) ni sh. 152 toka sh. 156 ya hapo awali.
Bei mpya kwa wafanyabiashara wa kati ni sh.157 toka sh. 159. Wanaonunua kwa wingi (bulk) ni sh. 152 toka sh. 156 ya hapo awali.
No comments:
Post a Comment