Serikali kupitia wizara ya viwanda,Biashara na
uwekezaji imeyataka makampuni yanayozalisha bidhaa nchini kusajili nembo za
bidhaa zao ili kuweza kupata takwimu sahihi ya bidhaa zizalishwazo
Nchini.
Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda,Biashara
na uwekezaji, Mkurugenzi wa uhamasishaji masoko katika Wizara hiyo Bw.Odilo Majengo
amesema hatua hiyo itapanua zaidi soko na kuitangaza Tanzania kwa uzalishaji wa
bidhaa kwa mataifa mengine.
Yote hayo yalizungumzwa katika hafla ya kusaini makubaliano
ya ushirikiano kati ya shirika la viwango Tanzania TBS na kampuni ya GSI Tanzania
Ltd yenye jukumu la kusimamia alama za utambuzi wa bidhaa.
Katika hatua nyingine pia kampuni ya GSI Tanzania Ltd
ambayo pia inahudumia nchi jirani za Rwanda,Burundi,Uganda,Zambia na Malawi
ilikabidhi vyeti kwa wazalishaji 14 walioojiunga na huduma za kampuni hiyo kwa
robo ya kwanza ya mwaka 2016
No comments:
Post a Comment