Halmashauri
ya wilaya ya Geita mkoani hapa imedhamiria kuboresha vituo vya afya ili kuweza kutoa
huduma zinazolingana na hospitali ya wilaya ili kupunguza idadi ya vifo vya
akina mama wajawazito pamoja na watoto.
Yayo yamesemwa na mkurugenzi wa halmashauri ya
wilaya ya Geita bw,Ally Kidwaka katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Musanyenge
ndani ya mji wa Katoro ambapo ameeleza kuwa kutokana na kuwepo kwa ongezeko kubwa la idadi ya watu katika mji huo inatakiwa
kuwepo hospitali yenye hadhi ya wilaya.
Aidha Kidwaka ameongeza kuwa wameweka mipango madhubuti
ya kuboresha vituo vya afya ambapo wataanza na vituo 2 wilayani hapa ikiwemo kituo cha afya Katoro pamoja na kituo
cha afya kilichopo Nzera.
No comments:
Post a Comment