Mfanyabiashara wa mazao, Eliusta Peter(40), amefariki dunia baada
ya kuchomwa na kitu chenye ncha kali shingoni akiwa katika nyumba ya
kulala wageni wilayani Kilombero.
Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Morogoro, Ulrich Matei alisema tukio hilo lilitokea Aprili
22 baada ya wahudumu wa nyumba ya wageni ya Sayari
kubaini maiti katika chumba namba mbili.
Inadawa Aprili 20
mwanamke huyo akiwa na kijana mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa
kwa ajili ya uchunguzi, walifika kwenye nyumba hiyo na kuchukua chumba kimoja
wakisema wao ni wafanyabiashara wa mazao.
“Mwili wa marehemu uligundulika ukiwa kwenye
nyumba ya kulala wageni iitwayo Sayari chumba namba mbili saa 11
jioni na ulipochunguzwa ikagundulika kuwa kifo kilisababishwa maumivu ya
jereha,”alisema Matei.
Mwanamke huyo
alikuwa na jeraha kushoto mwa bega lake lililotokana na kuchomwa na
kitu chenye ncha kali
Matei alisema
kwa taarifa walizozipata bila shaka kijana aliyekuwa naye anahusika
na mauaji hayo.
Wakati huo huo, jeshi
la polisi wilayani Kilosa limemkamata Rogasian Jeremia kwa tuhuma za
kumshambulia mkewe, Faustina Sizayi(25) kwa kumkatataka kwa mapanga
sehemu mbalimbali za mwili wake.
Mtuhumiwa alikamatwa
akiwa anajihusisha na kazi ya ulinzi wa maduka baada ya polisi kumsaka kwa muda
mrefu na ndipo Aprili 24 alikamatwa baada ya polisi kupata
taarifa kutoka kwa wasamaria wema.
No comments:
Post a Comment