Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania imesema iko katika hatua za
mwisho za uundaji wa kitengo maalum kitakachokuwa kikidhibiti maadili ya
utangazaji nchini ili kuhakikisha maadili ya Mtanzania yanalindwa.
Adhima hiyo ya Serikali kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
imetolewa Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Kamati ya Maudhi ya TCRA,huku
ikisisitiza lazima sheria za utangazaji zifuate ili kulinda maadili ya
Tanzania.
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Dkt Ally Simba amesema uwepo wa Kamati
ya Maudhui ndani ya TCRA ni muhimu katika kuhakikisha wanadhibiti ukiukwaji wa
sheria za utangazaji.
Kamati hiyo ambayo ni ya Nne kuuundwa kwa nyakati tofauti
inaongozwa na Prof, Haji Semboja, ambapo pamoja na masuala mengine
imemhakikishia Waziri huyo wa Habari nchini kuwa itajitahidi kuhakikisha
inaangalia namna ya uboreshaji wa tasnia ya habari nchini.
Awali Waziri huyo wa Habari alipata fursa ya kutembelea
Makumbusho ya Mawasilinao ya TCRA ambayo imesheheni vifaa vya zamani vya
utangazaji, kama vile simu, luninga, radio, ambapo vifaa vya zamani vya
utangazaji vya ITV, pia vimehifadhiwa ndani ya makumbusho hiyo.
No comments:
Post a Comment