Raia wawili wa China,
Ma Jun na Huifang Ma leo wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala kujibu
mashtaka mawili likiwamo la kushindwa kutumia Mashine ya Kodi za
Kielektroniki (EFDs) katika biashara zao.
Jun na Ma, ambao wote
ni wafanyabiashara na wakazi wa Mtaa wa Narung’ombe eneo la Kariakoo
wanakabiliwa na kushindwa kutumia mashine za EFDs pamoja na kushindwa
kujisajili katika kodi ya ongezeko la Thamani(Vat) wakati wakijua kufanya hivyo
kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.
Hata hivyo, mshtakiwa
wa kwanza katika kesi hiyo, Jun hakuwepo mahakamani hapo kwa madai kuwa yupo
nje ya nchi na upande wa mashtaka umeiomba Mahakama kutoa hati kwa ajili ya
kumkamata mshtakiwa huyo.
Akisoma hati ya
mashtaka, mbele ya Hakimu Mkazi Mwanadamizi Mfawidhi wa mahakama hiyo Said
Mkasiwa, Wakili kutoka Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), Cherubin Chuwa alidai
kuwa washtakiwa kwa pamoja walitenda makossa hayo Machi 23,mwaka huu.
Chuwa alidai siku hiyo
ya tukio, washtakiwa hao ambao wanamiliki Kampuni ya HM Textile Co
Ltd Iliyopo block 54 katika kiwanja namba 6 kilichopo mtaa wa
Agrey eneo la Kariakoo, walishindwa kutumia mashine za EFDs kwa
ajili ya kutoa risiti kwa wateja wao ambao walikuwa wanafanya manunuzi
mbalimbali katika duka hilo ambalo linauza mapazia na nguo mbalimbali, huku
wakijua kuwa ni kosa kisheria.
Mwandesha Mashtaka
huyo aliendelea kudai kuwa, katika shitaka la pili ambalo pia linawakabili
washtakiwa wote, inadaiwa kuwa muda na siku hiyo hiyo katika duka hilo,
washtakiwa walishindwa kujisajili katika kodi ya ongezeko la Thamani(Vat)
wakati wakijua kufanya hivyo kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.
Chuwa alidai
washtakiwa hao walishindwa kujisajili katika Kodi ya Ongezeko la Thamani(Vat)
ambayo ni kinyume cha sheria , na kwamba mashtaka hayo yamefunguliwa kupitia
sheria za TRA.
Hata hivyo mshtakiwa
wa pili, Huifang alikiri shtaka la kwanza huku shtaka la pili
akikana kuhusika.
Kutokana na hatua hiyo
wakili Chuwa alisema dhamana ya mshtakiwa huyo iko wazi ambayo ni kuwa na
wadhamini wawili kila kutoka taasisi inayotambuliwa kisheria watasaini bondi ya
Sh 3milioni na kuwasilisha mahakamani hati yake ya kusafiria.
Mshtakiwa huyo
alishindwa kutimiza masharti ya dhamana na kurudishwa rumande hadi April 21,
mwaka huu.
No comments:
Post a Comment